Na. Shinyanga RS
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme amepokea UJUMBE wa MKANDARASI kutoka Kampuni ya Sinohydro Corporation ya nchini China ukiongozwa na Mhandisi Emmanuel Anderson ambaye ni Meneja Mradi wa UMEME WA JUA TANESCO Makao Makuu ambao wamekuja kujitambukisha rasmi kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo kutumia unaojulikana kama SOLAR PHOTO VOLTAIC katika Kijiji cha Ngunga Kata ya Talaga Wilayani Kishapu hapa Mkoa wa Shinyanga.
Akitoa salamu za Serikali Mhe. Mndeme alimempongeza sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada zake kwa wananchi wa Tanzania hususani wa Mkoa wa Shinyanga kwa kuwezesha mradi huu hyjky akiwakaribisha tena kwa mikono miwili katika Mkoa wa Shinyanga.
“Wananchi wa Mkoa wa Shinyanga tunampongeza sana kwa kuendelea kutuhudumia na kutuletea maendeleo ambapo sasa tunakwenda kushuhudia ujenzi huo muda siyo mrefu ikiwa ni mradi wa jumla ya Megawatts 150, karibuni sana na katika hili niseme tu kuwa Serikali ipo nanyi bega kwa bega na kwamba itawapatia ushirikiano mkubwa wakati wote mtakapokuwa hapa.
Ikumbukwe kuwa huu ni mradi mkubwa zaidi wa umeme jua kuwahi kutokea Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki unatekelezwa katika Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga ambapo unatarajiwa kukamilika Agosti 2024.
|
|
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa