Na. Shinyanga RC.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme amepongeza sana uwekezaji sekta ya viwanda uliofanyika na unaoendelea katika mkoa wa shinyanga huku akipiga nduru kwa wawekezaji wengine kuja kuwekeza mkoa wa shinyanga kwakuwa kuna mahitaji yote muhimu kwa uwekezaji wa aina yoyote.
Mhe. Mndeme amesema hayo leo tarehe 21 Novemba, 2023 alipotembelea kiwanda cha Jambo Food Production C. Ltd kinachozalisha bidhaa za maji, juisi, biskuti, mikate na nyingine nyingi za chakula na Gilitu Enterprises Co. Ltd kinachozalisha mafuta ya kupikia ( SANICO), mchele na unga wa ugali viwanda vyote hivi vipo Manispaa ya Shinyanga.
"Kwa dhati ya moyo wangu nipongeze sana uwekezaji huu mkubwa unaofanywa na wazawa hawa, jambo ambalo linatia moyo na faraja kubwa kwa serikali kwakuwa wanazalisha ajira, wanalipa kodi stahiki, na wanauheshimisha mkoa na nchi kwa ujumla wake, hongereni sana Jambo na Gilitu," alisema Mhe. Mndeme.
Huu ni Utaliiwa Viwanda Mkoa wa Shinyanga, ambapo Mhe. Mndeme ametoa wito kwa wadau na woye wenye nia ya kujifunza watembelee shinyanga waje kuona uwekezaji bora, wenye tija, wenye kuvutia uliopo hapa shinyanga, hakika shinyanga ya sasa siyo ya zamani.
Aidha serikali imeahidi kuwapatia ushirikiano wa kutosha wawekezaji hawa, waliopo, watakaokuja wawe wazawa au wageni serikali itawawekea mazingira rafiki wakati wote na hayo ndiyo maelekezo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo waje kuwekeza shinyanga.
Huu ni muendelezo wa ziara za Mhe. Mndeme ndani ya mkoa ambapo anaangalizia na kuhamasisha uwekezaji zaidi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM wa kuhakikisha maendeleo yanawafiiia wananchi vyote kupitia uwekezaji uliopo shinyanga hasa katika sekta ya viwanda, elimu nk huku akiitaja ziara hii kuwa ni UTALII WA VIWANDA MKOANI SHINYANGA.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa