Na. Shinyanga RS.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ameshiriki katika sherehe ya kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari KOM ilyopo Manispaa ya Shinyanga na kuagiza wazazi na walezi wote kuwalea Watoto kwa kuzingatia maadili yetu ili wasije kuiga ya nchi za nje ambayo hayaendani na utamaduni wetu huku akiwataka kuwawekea akiba Watoto wao katika Benki ya CRDB kupitia akaunti maalumu ya JUNIOR JUMBO ACCONT (JJ).
Hayo yamesemwa leo na tarehe 18 JUNI, 2023 wakati akizungumza na watoto pamoja na wazazi/walezi wao kwenye sherehe hiyo iliyoandaliwa na Benki ya CRDB na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kamati ya Usalama, wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, waalimu na uongoz wa Shule ya Sekondari KOM.
Mhe. Mndeme alisisitiza sana suala la maadili kuwa kumekuwa na mmomomyoko mkubwa sana wa maadili hasa kwa Watoto na vijana wa kiume jambo ambalo linapelekea kuhatarisha usalama wa kizazi cha sasa na maadili ya Taifa jambo ambalo amesema ni hatari na kwamba wazazi sasa wanao wajibu mkubwa wa kulinda, kukemea, kuelimisha na kusimamia Watoto wetu.
“Sote tunafahamu kuwa hivi sasa Dunia imekuwa Kijiji kimoja, hii ni kutokana na muingiliano wa tamaduni za mataifa mbalimbali na sisi kama watanzania tunazo tamaduni zetu ambazo tumezirithi kutoka kwa mababu zetu, hivyo nitoe wito kwa wazazi na walezi Mkoa wa Shinyanga tuzienzi nz kuzitunza na kuzidumisha tamaduni zetu,” alisisitiza Mhe. Mndeme.
Awali akitoa taarifa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ambaye ndiye mgeni rasmi Kaimu Meneja Kanda ya Magharibi Ndg. Jumanne Wagana alisema kuwa, katika kuadhimisha siki ya mtoto wa afrika CRDB MKOA WA SHINYANGA waliamua kushirikiana na uongozi wa Shule ya Sekondari ya KOM.
Wagana alimueleza mgeni rasmi kuwa katika kuadhimisha sherehe hizi CRDB inayofuraha kubwa kuwaarifu wazazi na walezi wote Mkoa wa Shinyanga kuwafungulia Watoto wao Akaunti Maalumu ya Junia Jumbo Akaunti (JUNIOR JUMBO ACCOUNT) akaunti ambayo mtoto atawekewa fedha zake , kwa ajili jambo maalumu kama vile kulipia ada nk lakini pia haina makato, na inayo riba au faida ambayo mzazi au mlezi ataipata kupitia akaunti hiyo ambayo inatajwa kuwa mkombozi kwa elimu ya watoto wote.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa