Na. Shinyanga RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme leo tarehe 7 Julai, 2023 ameshiriki katika Tamasha la Sanjo Busiya ambalo limefanyika katika Kijiji cha Negezi Kata ya Ukenyenge Wilaya ya Kishapu hapa Mkoani Shinyanga na kuwapongeza sana waandaaji kwakuwa tamasha hili limeanza rasmi tarehe 1 Julai, 2023 na linatajwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya 10,000 kutoka pande mbalimbali na kwamba huu ni mwaka wa 13 tangua kuanzishwa kwa tamasha.
Pamoja na pongezi nyinhi kwa ma Chifu na uongozi wote kwa kufanikisha sherehe hizi lakini pia amewasihi kukemea kwa nguvu zote mmomonyoko wowote wa maadili ambao unaweza kuharibu jamii yetu na vizazi vyetu kwa ujumla huku akiwakumbusha watambue kazi njema anayoifanya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwamo afya, elimu, miundombinu, ustawi wa jamii huku akiwataka kumuunga mkono kwa kazi zote za kuwaletea maendeleo wananchi.
"Ndugu zangu wanaTamasha la Busiya nawapongeza sana kwa kufanikisha vema sana tamasha hili muhimu ambalo limehudhuriwa na watu zaidi ya elfu kumi kutoka ndani nan nje ya Mkoa wa Shinyanga, lakini pia niwakumbushe ndugu zangu kuendelea kusimamia maadili yetu ya Kitanzania na tuendelee kumuunga mkono Rais wetu kwa kazi kubwa na njema ambazo anazifanya katika kutuletea maendeleo sisi wananchi," alisema Mhe. Mndeme.
Serikali imepokea changamoto zote zilizowasilishwa na Chifu Edward na kwamba zitashulikiwa kulingana na zilivyo kwakuwa zipo za kisera na kibajeti.
Kwa upande wake Mtemi wa Busiya Ndugu Edward Makwaiya aliipongeza sana Serikalikwa kazi inazozifanya kwa wananchi huku akiomba Serikali kuanzisha Chombo Maalumu kiwe na Mamlaka kama zilivyo Mamlaka nyingine ili waweze kuwa na maamuzi katika kuisaidia Serikali kupambana na mila potofu zenye kuharibu jamii.
Aidha Mtemi Mwakwaiya alisema kuwa lengo la tamasha hili ni pamoja na kumshukuru Mungu kwa mwaka uliopita, na kukaribisha mwaka mwingine ikiwa ni pamoja na kudumisha tamaduni zetu na kuwaelimisha wananchi wote kuacha kuiga utamaduni wa nje na kuhamasisha utalii wa ndani kwa mashindano ya ngoma za jadi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa