Na. Shinyanga RS.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme Septemba 20, 2023 amesikiliza na kutatua papo hapo kero za wananchi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Shunu Kata ya Nyahanga Manispaa ya Kahama.
Akizungumza katika mkutano huo Mhe. Mdeme mesema baadhi ya kero zilizowasilishwa na wananchi zimeanza kushughulikiwa ikiwamo ya ubovu wa miundombinu ya barabara ambaopo fedha zinaendelea kutolewa na ujenzi unaendelea.
Kero ya maji ilipatiwa ufumbuzi papo hapo ambapo alimuagiza Mkuugenzi wa Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Kahama Ndg. Allen Marwa kulishughulikia kwa haraka suala la kubadilisha mtandao wa bomba za zamani na kuweka mpya, huku suala la migogoro ya ardhi akimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Ndg. Anderson Msumba ili kuliondoa haraka na wananchi waendelee na shughuli zao za maendeleo.
Sanjari na hilo, kuhusu Kero ya Shule ya Sekondari kwa eneo hilo la Nyahanga kwa sasa Serikali inamalizia ujenzi wa Shule mpya ya Nyahanga inayogharimu zaidi ya milioni 603 huku akiwaeleza kuwa amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama kuongeza shule nyingine kupitia bajeti ijayo.
Mhe. Mndeme amesema katika Mkoa wa Shinyanga pekee, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi shilingi Trilioni moja ndani ya utawala wake fedha ambazo zitatumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha, amewasihi pia wananchi waendelee kumuunga Mkono Rais Samia ili aendelee kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Awali baadhi ya wananchi waliowasilisha kero zao kwenye mkutano huo ambazo zilipatiwa majibu na RC Mndeme.
PICHA NA MATUKIO KATIKA MKUTANO WA HADHARA NYAHANGA - KAHAMA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa