Na. Shinyanga RS
MKUU wa mkoa wa shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme amewataka wafanyabiashara ya usafirishaji abiria na mizigo kupitia pikipiki (Bodaboda) kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuwafichua wahalifu ili kuweza kutokomeza kabisa uhalifu katika maeneo yao huku akiwasisitiza kuendelea kuzingatia na kutii sheria za barabarani kwakuwa kazi zao zinahusisha wananchi.
Mhe. Mndeme ameyasema hayo leo alipomuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Dkt. Yahaya Nawanda kama mgeni rasmi kwenye mashindano ya bodaboda yaliyopewa jina la Polisi Bodaboda Marathon -Simiyu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni ya Sema Nao iliyoanzishwa na Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu sambamba na kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwl . Julius Kambarage Nyerere akitimiza miaka 24 tangu kifo chake.
"Pamoja na kuwapongeza sana nyote kwa kuandaa mashindano haya, lakini niwatake bodaboda wote kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika zoezi la kuwafichua wahalifu wote ili tuweze kutokomeza kabisa uhalifu katika maeneo yetu, pia muendelee kuzingatia sheria wakati wote wa kazi zenu kwakuwa zinahusisha wananchi na mali zao," alisema Mhe. Mndeme.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishna Msaidizi wa Polisi Edith Swebe alimueleza kaimu mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Mndeme kuwa uwepo wa hadhara hii unajieleza namna ambavyo jeshi la polisi lilivyo na ushirikiano mzuri na wananchi wakiwemo bodaboda wenyewe huku akisema kuwa hafla hii ni sehemu ya utekelezaji wa Kampeni ya Ongea Nao iliyoanzishwa maalum kwa ajili ya kujadili na kutatua kero zao.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Mndeme alimuwakisha mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Dkt. Yahaya Nawanda ambaye hakuweza kushiriki kwakuwa hakuwepo katika maadhimisho haya ambayo yamefanyika tarehe 14 Oktoba, 2023 ikiwa ni sehemu pia ya kumuenzi baba wa taifa Hayati Mwl. J.K Nyerere.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa