Na. Shinyanga RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewataka wananchi Mkoani Shinyanga kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 ambapo utqpokelewa katika Shule ya Msingi Buganika iliyopo Wilaya ya Kishapu ukitokea Mkoani Simiyu.
Mhe. Mndeme ameyasema hayo leo tarehe 26 Julai, 2023 Ofisini kwake alipokuwa akiongea na wa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kupitia vyombo vya habari ambapo amewaeleza kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani Shinyanga utakimbizwa Kilomita 571.5 kuweka mawe ya msingi, kuona miradi, kufungua pamoja na kuzindua miradi 41 yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 14.
"Nitumie nafasi hii kuwaomba wananchi wote wa Mkoa wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya Shule ya Msingi Buganika Wilayani Kishapu kwa ajili ya kupokea Mwenge, pia mjitokeze kwa wingi kwenye miradi yetu yote ambapo Mwenge wa Uhuru utafika ili kutoa hamasa na kuonesha upendo wetu unaoambatana na uzalendo kwa wakimbiza Mwenge na kwa wale watakaokwama kufika basi wajipange pembezoni mwa barabara ambapo Mwenge utapita wakiwa na majani kuoneaha AMANI IPO," alisema Mhe. Mndeme.
Mwenge wa Uhuru utapokelewa Mkoani ShinyangaTarehe 27 Julai, 2023 ukitokea Mkoa wa Simiyu na utakabidhiwa tarehe 2 Agosti, 2023 Mkoani Geita.
Kauli Mbiu: Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe hai na Uchumi wa Taifa.
Picha ikionesha wanahabari wakati wa mkutano ndani ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa