Na. Shinyanga RS
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme amezindua rasmi Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria kwa Mkoa wa Shinyanga pamoja na kumshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kampeni hii huku akitoa agizo kwa kila Kata kutenga Chumba Maalumu kwa ajili ya kuhudumia masuala yote yahusuyo msaada wa kisheria.
Mhe. Mndeme ambaye alikuwa mgeri rasmi wa hafla ya uzinduzi huu ameyasema leo tarehe 11 Juni, 2023 katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo Manispaa ya Shinyanga hafla iliyohudhuriwa na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa kiserikali, dini na Chama cha Mapinduzi kutoka katika Wilaya zote za Mkoa huku akiwataka wananchi kujitokeza kuzitumia vema siku hizi 10 na kuwapa ushirikiano wataalamu wanaokwenda kutoa huduma kwao katika kila Vijiji 3 na Mitaa 3 kutoka kwenye kila Kata.
"Nawaagiza viongozi wote katika kila Kata kuhakikisha wanatenga chumba maalumu kwa ajili ya kutoa huduma za msaada wa kisheria, lakini pia nitumie nafasi hii kuwataka viongozi wote kwenda kuhamasisha wananchi wajitokeze kuhudumiwa katika kipindi hiki maalumu cha siku 10 na muwatangazie waziwazi kwamba huduma hii ni bure kabisa hakuna malipo yoyote," alisema Mhe. Mndeme.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Poline Gekulu alimshukuru sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kutumia jina lake katika kampeni hii huku akimshukuru pia kwa kutenga fedha nyingi kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wengi wasiokuwa na uwezo wa kutetea haki zao katika kwro za Ardhi, Ndoa, Mirathi na Usia na kwamba wanakwenda kuwafikia walengwa wote huku akiwaomba viongozi wote kuendeleza utaratibu huu wa kutatua kero za wananchi hata baada ya kampeni hii kuisha muda wake.
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imezinfuliwa rasmi katika Mkoa wa Shinyanga ukiwa ni Mkoa wa 3 Kitaifa kuzindua baada ya Dodoma na Manyara na sasa Mkoa wa Shinyanga kampeni ikiwa na lengo mahsusi la kutatua kero za Mirathi, Ndoa, Mali, Urithi pamoja na changamoto zote zinazowagusa wananchi.
Picha zikimuonesha Mhe. Christina Mndeme, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Poline Gekulu na baadhi ya viongozi wakitembelea na kusikiliza kero mbalimbali kutoka kwa wananchi waliojitokeza wakati wa uzinduzi wa kampeni.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa