Na. Shinyanga RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme ameweka Jiwe la Msingi katika ujenzi wa Tangi la Maji lenye ujazo wa Lita 100,000 pamoja na bomba kuu la maji lililojengwa kwa ushirikiano wa Life Water International pamoja na RUWASA utaohudumia Vijiji 4 vya Mwalukwa, Bulambila, Kadoto na Ng'hama na kuhudumia wananchi zaidi ya 8400 na jumla ya mtandao wa KM 34 mradi ambao umetekelezwa katika Kijiji cha Bulambila Kata ya Mwalukwa.
Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi Mhe. Mndeme amesema, Serikali ya awamu sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inauhusiano mzuri sana na Mashirka yasiyo ya Kiserikali na ndiyo sababu leo tunashuhudia kukamilishwa utekelezaji wa mradi huu muhimu ambao umekuja kuondoa kero hapa Kata ya Mwalukwa huku akiwataka Life Water International na RUWASA kuona namna ya kuongeza Tangi na mtandao wa maji zaidi ili uweze kuwahudumia watu wegi zaidi.
"Nawapongeza sana Life Water International na RUWASA kwa kutekeleza mradi huu mkubwa kabisa uliogharimu zaidi ya Bilioni 1 na ambao unaondoa na kutatua kero za uhaba wa maji kwa wananchi zaidi elfu 8484 ukiwa ni mtandao wenye urefu wa KM 34, hakika ni furaha sana hata wananchi mmewasikia hapa wakimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha ukamilikaji wa mredi huu", alisema Mhe. Mndeme.
Kando na mradi huu, Mhe. Mndeme pia alitembelea na Ukarabati wa Bwawa la Mwalukwa ambalo awali lilikuwa na kina cha Mita 2.25 na sasa litakuwa na kina cha Mita 4.1 ambapo kwa upande wa ujazo wa lita za maji awali lilikuwa ni zaidi ya lita elfu 71 na litakapokamilika litakapokamilika litakuwa na uwezo wa lita zaidi ya laki 2.93.
Ukarabati huu wa Bwawa unakwenda kuwanufaisha wananchi zaidi ya elfu 22 ambao watawekea Birika kwa ajili ya kutumia maji haya na mifugo zaidi ya 13 ambapo kutaondoa kabisa kero ya uhaba wa maji eneo hili.
Ziara ya Mhe. Mndeme imehitimishwa kwa kufanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mwalukwa ambapo alisikiliza na kutatua kero za wananchi huku kubwa zaidi ikiwa ni kucheleweshwa kwa ukamilikaji wa bwawa hilo, ukosefu wa nyumba za walimu na ucheleweshaji wa usambazaji wa umeme wa REA.
Kero zote zilitatuliwa papo hapo ambapo suala la uchelewesha wa mradi aliagizwa msimamizi kukamilisha haraka ifikapo tarehe 15 Oktoba, 2023, kero ya nyumba ya walimu alimuagiza Mkuu wa Wilaya kulishughulikia huku kero ya REA akimueleza mwananchi kuwa umeme utawafikia hivi karibuni kwani ni jana tu ambapo mkandarasi alikutana na Mhe. Mndeme akamuahidi kufikisha huduma hiyo mapema Oktoba, 2023.
Huu ni muendelezo wa ziara za Mhe. Mndeme za kukagua utekelezaji wa miradi, kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Halmashauri zote 6 za Mkoa wa Shinyanga ambapo leo iilkuwa ni zamu ya Shinyanga DC.
MATUKIO KATIKA PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa