Leo Oktoba 29, 2025, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita @mboni_mhita ameongoza maelfu ya wananchi wa Mkoa huo kushiriki katika zoezi la kupiga kura, kutimiza haki yao ya kikatiba kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani.
Baada ya kupiga kura kwenye kituo cha Kahama Mjini, Mhe. Mhita ametoa wito kwa wananchi wote waliopo kwenye daftari la wapiga kura kujitokeza kwa wingi, kwa amani na utulivu, kuhakikisha wanashiriki katika kuamua hatma ya uongozi wa Taifa.
Hata hivyo Mhe. Mhita amesema mpaka sasa hakuna tishio lolote la kiusalama hivyo wananchi waendelee kujitokeza kupiga kura.
OFISI YA MKUU WA MKOA, MKOA WA SHINYANGA, 04 MTAA WA BOMA
Anuani: P.O.Box 320, 37180,SHINYANGA, TANZANIA
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa