Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Zainab Telack amewaonya wananchi wenye tabia ya kuchochea migogoro hususani ya ardhi inayopelekea uchonganishi kati ya Serikali na wananchi.
Telack metoa onyo hilo hapo jana tarehe 26/06/2019, alipofanya mkutano wa hadhara kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi uliofanyika kwenye uwanja wa Majengo, Halmashauri ya mji wa Kahama.
"Kahama ni vinara wa migogoro ya ardhi,lakini ni migogoro isiyokuwa na tija. Kuna watu wanachochea na wengine wamo ndani ya jeshi la polisi" amesema Telack.
Amesema anatoa onyo hilo na waache mara moja.
Aidha amemuagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kahama, kuhakikisha wahusika wa migogoro ya ardhi hususani kata ya Malunga wanahojiwa.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa