Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amewaonya wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa miradi mbalimbali Mkoani hapa kuwa makini na kazi wanazopewa na Serikali na kufuata maelekezo yaliyomo kwenye mikataba ya kazi.
Mhe. Telack ametoa onyo hilo mapema leo tarehe 21 Oktoba, 2019 wakati akikagua mradi wa ujenzi wa Dampo katika eneo la Nhelegani, Manispaa ya Shinyanga unaojengwa kwa shilingi milioni 484 na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu, chini ya Mkandarasi aitwaye Jonta Investment.
“Kazi ya Serikali iogope kama ukoma,ulichoambiwa kufanya fanya hivyo hivyo, kama kuna shilingi umeambiwa utoe ili utengeneze chini ya kiwango siyo kwa Mkoa huu” amesema Telack.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa