Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amezionya taasisi za fedha zinashikilia kadi za kutolea fedha za Watumishi wa Umma kinyume na utaratibu.
Onyo hilo amelitoa mapema leo tarehe 04 Mei, 2019 akiwa na Kamati za Usalama za Mkoa na Wilaya ya Shinyanga katika Ofisi ya Mara Credit Co Ltd (MCCL) inayojihusisha na kukopesha watumishi na watu binafsi kisha kuchukua kadi zao za benki na namba za siri kwa lengo la kutoa fedha mishahara ya watumishi hao itakapoingia.
Taasisi hiyo iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga, imekutwa na kadi za watumishi za kutolea fedha benki zaidi ya 267 pamoja na kadi za bima za afya, vitambulisho vya kazi na vitambulisho vya kupigia kura.
Mhe. Telack amesema taasisi hizo zinaweka masharti rahisi ili waweze kuwaibia watumishi wa Umma wakijua kabisa wanafanya hivyo kinyume na taratibu na biashara hiyo hata kwa watu binafsi ikomeshwe.
Amezitaka pia Benki Mkoani hapa kuhakikisha wanasimamia suala la watu kwenda kwenye mashine za kutolea fedha kwa kadi tofauti kupitia kamera zao ili kuwabaini watu hao.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa