Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amesema kuwa Serikali ipo tayari kuahirikiana na Uongozi wa Shycom Alumni Marathon 2024 na kuyafanya mashindano haya kuwa ya Kimataifa ambapo itaweza kuitangaza vema SHYCOM yenyewe, Shinyanga na Tanzania kwa ujumla kwani itajumlisha wakimbiaji kutoka ndani na nje ya Nchi pia.
Shycom Alumni Marathon 2024 ni mbio za hisani ambao zimeandaliwa na waliokuwa wanafunzi wa Chuo hicho ambacho awali kilikuwa Chuo cha Biashara na sasa ni Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM)
RC Macha ameyasema haya leo tarehe 21 Septemba, 2024 baada ya kukamilika kwa mbio hizi za hisani ambazo zimejumuisha wakimbiaji wa Kilometa 5, 10 na 21 na kisha kufungua mashindano ya mbio za baiskeli huku yeye RC Macha na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni wakishirki mbio za Kilometa 5 ambapo pia ametumia nafasi hii kuwapongeza wandaaji wote wa michezo hii na kusisitiza kuwa uwepo wa tukio hili hapa mjini limeongeza mzunguko wa fedha.
"Kupitia mbio hizi za hisani kuwa, Serikali inatambua na kuthamini sana uwepo wa michezo kwa wananchi wake, na hivyo niseme tu kwamba Serikali ipo tayari kushirikiana na Uongozi wa Shycom Alumni Marathon ili kuyafanya mashindano haya kuwa ya Kimataifa jambo ambalo litaitangaza vema Shyco, Mkoa wa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla," amesema RC Macha.
Akizungumza na wanahabari mlezi wa mashindano haya ambaye pia ni mmoja wa wanafunzi waliosoma Shycom Prof. Mussa Assad amesema kuwa uwepo wa Shycom Alumni Marathon hapa mkoani Shinyanga ni kukienzi Chuo, kukusanya fedha kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya Chuo hiki na kuwezesha wanachuo wengine kuendelea kunufaika na Chuo hiki ambacho kimekuwa na tija kubwa wa wengi zaidi.
SHYCOM ni Chuo ambacho kimetoa hazina kubwa ya wasomi hapa nchini akiwamo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hhesabu za Serikali (CAG), Profes Charles Kichere, Prof Mussa Assad na wengine wengi zaidi kama walivyojitokeza leo huku wakitajwa kwa kuonesha uzalendo, wenye kujitoa na mfano wa kuigwa na wengine ambao wanaweza kurejesha fadhira kwa shule na vyuo walivyosoma.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa