SERIKALI ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA JUMUIYA YA MARIDHIANO NA AMANI - RC MACHA
Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amekutana na kufanya mazungumzo na Jumuiyw ya Maridhiano na Amani Mkoa wa Shinyanga ambapo pamoja na kupokea taarifa yao lakini pia amewaeleza kuwa Serikali inatambua, inathamini na kuheshimu kazi zote zinazofanywa na Jumuiya na kwamba inaendelea kushirikiana nao wakati wote huku akisisitiza kuwa mlango wa Mkuu wa Mkoa upo wazi kwao wakati wote wanapohitaji jambo lolote wafike.
RC Macha ameyasema haya tarehe 15 Mei, 2024 alipokutana nao ofisini kwake ambapo walifika kwa lengo la kujitambulisha kwake na kuelezea kazi wanazozifanya hapa Mkoani Shinyanga huku wakitoa pongezi zaidi kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri anayoifanya kwa kuwaletea maendeleo Watanzania wote wakiwemo na Wanashinyanga kupitia vijiji vyote 506 ambapo kupitia Sekta mbalimbali vimefikiwa.
Jumuiya ya Maridhiano na Amani ambayo inaongozwa na Mwenyekiti wake Sheikh Khamis Balilusa wamemuahidi ushirikiano wote Mhe. Macha na kwamba wataendelea kufanya kazi na Serikali wakati wote katika kuhakikisha jamii inanufaika na uwepo wa Baraza.
Jumuiya ya Maridhiano imekuwa na mchango mkubwa sana kwa Serikali ambapo limekuwa likisaidia katika nyanja mbalimbali za utoaji elimu na hamasa kuhusu maadili bora, elimu ya dini, katika nyanja za mila na kabila, utoaji wa tadhari dhidi ya mambo mbalilmbali kupitia hadhara, vikao na nyumba za dini kwa lengo la kuiweka sawa jamii ya Wanashinyanga na Watanzania kwa ujumla.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa