Na. Shinyanga RS
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme leo tarehe 6 Novemba, 2023 amewatembelea wahanga wa maafa walioezuliwa na kubomolewa makazi yao katika kata ya Kizumbi na Mwamala kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia terehe 6 Desemba, 2023.
Akizungumza na wahanga hao Mhe. Mndeme amewapa pole sana na kuwaeleza kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imepokea kwa masikitiko makubwa taatifa za mafuriko haya na kwamba sasa serikali itatoa huduma ya matibabu bure mpaka kupona kwa majeruhi wote, italeta mbegu kwa waathirika wa mashamba, italeta vifaa vya kulalia na itafanya tathimini ya awali ili kujuwa kiasi cha hasara iliyopatikana na mahitaji halisi.
"Poleni sana ndugu zetu kwa tukio hili, lakini tu niseme kuwa serkali itagharamia matibabu wa majeruhi, kuleta mbegu, vifaa vya kulalia, pia nimuagize Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga kufanya tathimini ya awali kujuwa uhalisia wa mahitaji na hasara iliyopatikana ili serikali ijue, niseme tu kuwa, haya ndiyo maelekezo ya Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wahanga wote," alisema Mhe. Mndeme.
Awali akitoa taarifa ya hali ilivyokuwa, Diwani wa Kata ya Kizumbi Mhe. Reuben Kitinya alisema kuwa, mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia tarehe 6 Desemba, 2023 iliyoambatana na upepo mkali pamoja na barafu ndiyo iliyoleta athari yote hiyo huku akisema jumla ya nyumba 31 zimeathirika kwa kung'olewa bati na kaya 27 kubomoka kabisa na hivyo kupelekea wananchi hao kuombewa hifadhi kwa ndugu na jamaa.
Aidha kwa Kata ya Mwamala jumla ya nyumba 51 zimeathirika na mvua hizo pamoja na hekari takribani 10 kuharibiwa kabisa na mvua ya barafu iliyoambatana na upepo mkali katika kijiji cha Ibanza sanjali na kuumiza watu wanne akiwemo bibi kizee ambaye amelazwa hospitali ya Mwawaza.
Mhe. Mndeme ametoa wito kwa wananchi wote kuendelea kuchukua tahadhari ya mvua hizi zilizotabiriwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa kuwa zitakuwa za juu ya kiwango, kuondoka maeneo yote hatarishi.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa