Serikali imesema itaendelea kusimamia na kusisitiza suala la kuwa na Maktaba kwa kila shule ya Msingi na Sekondari ili kuhakikisha wanafunzi wote wanakuwa na tabia ya kujisomea na kusoma vitabu halali na sahihi badala ya kutegemea zaidi mitandao ya kijamii maarufu kama ku"google".
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack ameyasema hayo wakati akifungua Warsha na Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wakutubi (Wasimamizi wa Maktaba) unafanyika kwa siku nne katika Manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga.
Mhe. Telack amesema ni muda sasa wa kusimamia kila shule iwe na maktaba ili kuwasaidia wanafunzi kwani wengi wao wanapotumia mitandao hiyo wakati mwingine wanafeli mitihani kwa sababu hawapati majibu sahihi yanayotakiwa kutokana na kuwa kila mtu kwenye mitandao hiyo anaandika anavyofahamu.
Hali kadhalika, Mkuu wa Mkoa amewataka waandishi wa Habari kuwaelimisha wananchi kupitia vyombo vyao ili waelewe maana na kazi ya Wakutubi nchini na umuhimu wa kusoma vitabu.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa