• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

SERIKALI YA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN ITAENDELEA KUWATAMBUA, KUWATHAMINI NA KUWAHESHIMU WAZEE – RC MACHA

Posted on: June 14th, 2025

#Shinyanga_RS

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuwatambua, kuwathamini, kuwaheshimu na kuwatunza wazee wote nchini kwa kutambua mchango wao mkubwa katika ujenzi wa Taifa, kupitia uzoefu, mawazo na maarifa waliyonayo.

RC. Macha ameyasema hayo Juni 14, 2025, wakati akihutubia Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Kuelimisha na Kupinga Ukatili Dhidi ya Wazee Duniani, lililofanyika katika ukumbi CCM Mkoa wa Shinyanga. Kongamano hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, taasisi za dini, mila, Kamati ya Amani ya Mkoa, Baraza la Jumuiya ya Wazee, pamoja na wananchi.

“Serikali yetu inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuwathamini na kuwatunza wazee wote ili waendelee kufurahia maisha kama walivyo wananchi wengine. Wazee ni kundi muhimu, na ndio maana Serikali imeendelea kuhakikisha wanapatiwa kipaumbele katika huduma za kijamii, ikiwemo kuanzisha madirisha maalum ya kuwahudumia wanapofika katika vituo vya kutolea huduma za afya,” alisema RC Macha.

Kwa niaba ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Felister Mndemu, aliwasilisha salamu rasmi, akisisitiza umuhimu wa kuendeleza malezi bora kwa wazee kwa kuwajengea moyo wa huruma, heshima kwa wazee, na ushiriki katika shughuli za kuwatunza wazee katika jamii.

“Wazee siyo mzigo bali ni hazina yenye thamani kwa Taifa letu. Tunapaswa kuwakuza vijana wetu katika misingi ya maadili mema, utu na mshikamano ili kujenga jamii yenye heshima kwa wazee na kuheshimu mchango wao,” alisema Bi. Mndemu.

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Mkoa wa Shinyanga ulikuwa na watu 100,626 wenye umri wa miaka 60 na kuendelea, sawa na asilimia 4.5 ya watu wote katika Mkoa huo, ambao walifikia 2,241,299. Kwa mwaka 2025, idadi hiyo inakadiriwa kuongezeka hadi 101,114 kati ya watu 2,483,928, sawa na asilimia 4.1.


Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • TUTAENDELEA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI – RC. MACHA

    June 17, 2025
  • SERIKALI ITAENDELEA KUWALINDA WAZEE- NAIBU WAZIRI MWANAIDI

    June 15, 2025
  • SERIKALI YA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN ITAENDELEA KUWATAMBUA, KUWATHAMINI NA KUWAHESHIMU WAZEE – RC MACHA

    June 14, 2025
  • MKURUGENZI MKUU WA TANESCO AMKABIDHI MKUU WA MKOA WA SHINYANGA JIKO LA KISASA LA UMEME

    June 09, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa