Na. Shinyanga RS.
WAZIRI wa Madini Mhe. Anthony Mavunde (MB) leo akiwa katika ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ya mkuu wa mkoa wa shinyanga amepokea taarifa uchunguzi migodi ya wachimbaji wadogo Mwakitolyo yaliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinaynga huku akiwahakikishia kuwa hakuna mchimbaji yoyote atakayeondelewa katika eneo hilo.
Katika taarifa iliyofanywa na timu ya wataalamu kuhusu uchambuzi wa mikataba kati ya Vikundi vya wachimbaji wadogo wa madini na mwekezaji kwenye leseni za uchimbaji mdogo zilizopo katika eneo la Mwakitolyo mkoani Shinyanga kamati imebaini sehemu kubwa ya maduara hayapo katika hali salama ya uchimbaji.
Taarifa hiyo imebainishwa leo oktoba 11,2023 na mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi kutoka Wizara ya Madini Mhandisi Ally Samaje wakati akiwasilisha taarifa ya uchunguzi kwa Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde mkoani Shinyanga.
Mhandisi Samaje amesema kuwa katika kipindi cha kati ya mwezi Septemba 2022 hadi Oktoba 2023, mitambo 137 ya kuchenjulia dhahabu katika eneo la Mwakitolyo imezalisha takribani kilogramu 1,162 sawa na tani 1.162 , kati ya kiasi hicho kilogramu 639ambazo sawa na asilimia 55 imetoka katika eneo la Nyaligongo.
Akielezea kuhusu utaratibu wa kuingiza na kutoa malighafi zinazotokana na u chimbaji madini katika eneo la Mwakitolyo Mha.Samaje amesema idadi ya vibali 1578 vya uchimbaji madini vitolewa na kuzalisha tani 271,278 za mbale kutoka eneo la Nyaligongo.
Aidha , Mhandisi Samaje ameshauri kuwa Mkaguzi wa Migodi asimamie mpango maalumu wa uchimbaji madini kwa kufanya ukaguzi mara kwa mara pamoja na kuwashauri namna bora ya kuendesha shighuli za uchimbaji kwa usalama.
Kwa ujumla kamati ilibaini yafuatayo,
● Kamati yabaini maduara
hai 65 kati ya maduara 1297,
● *Ni maduara 6 tu yenye Uzalishaji kati ya maduara 134,
● Septemba 2022 hadi Oktoba 2023 tkribani kilogramu 1,162 za dhahabu zimetoka Mwakitolyo,
"VISION 2030" MADINI NI MAISHA NA UTAJIRI.
Eng. Ally Samaje Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguziWaziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde (MB) akiwa na Prof. Siza Tumbo (kushoto) ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga wakati wa mkutano wa wachimbaji wadogo katika ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ya mkuu wa mkoa wa shinyanga.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa