Serikali ya Mkoa wa Shinyanga imewashauri wadau wa afya Mkoani hapa kuanza kuwaelimisha wananchi kujikinga na maradhi mbalimbali badala ya kutumia fedha na nguvu katika kutibu.
Akifungua kikao cha siku mbili cha wadau wa afya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amesema wadau waelekeze nguvu kwenye kuzuia ili kuepuka kutumia gharama kubwa katika tiba. Amesema, "afya ndiyo mtaji wa kila kitu hivyo tufikirie kukinga watu wetu ili wawe wazalishaji badala ya kusubiri waugue tuwatibu"
Aidha, amewaomba wadau kutenga bajeti kwa ajili ya nyumba za watumishi hasa maeneo ya vijijini ambako kuna changamoto ya makazi kwa wa ajili ya watumishi wa afya.
Telack amesema kuwa, kila mdau akijenga nyumba moja watakuwa wameongeza nyumba 30 za watumishi ili wananchi wapate huduma kwa karibu na haraka kwani wananchi wanawahitaji sana watumishi hao.
Wakati huo huo, Telack ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Kahama kufuatilia na kumpima kila mgeni anayeingia Mkoani Shinyanga kupitia Wilayani humo katika kudhibiti ugonjwa wa Ebola ambao umeripotiwa kuwa katika nchi ya jirani ya Congo.
Amesema elimu itolewe kwa wananchi kujihadhari na kutoa taarifa watakapoona dalili au mtu mwenye dalili za ugonjwa huo.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa