Zikiwa zimesalia saa chache kuelekea Uchaguzi Mkuu, halmashauri zote sita katika wilaya tatu za Mkoa wa Shinyanga zimetekeleza kwa mafanikio zoezi la kupokea vifaa vya kupigia kura.
Kwa Mkoa wa Shinyanga, jumla ya vituo 3,313 vimeandaliwa kwa ajili ya kupigia kura. Wapiga kura 1,244,833 wanatarajiwa kushiriki katika zoezi la kumchagua Rais, huku 1,244,621 wakiwa wamejiandikisha pia kuchagua Wabunge na Madiwani.
Tunatoa wito kwa wananchi wote wenye sifa kujitokeza kwa amani na utulivu kutimiza haki yao ya kikatiba.
KURA YAKO, HAKI YAKO — JITOKEZE KUPIGA KURA!

OFISI YA MKUU WA MKOA, MKOA WA SHINYANGA, 04 MTAA WA BOMA
Anuani: P.O.Box 320, 37180,SHINYANGA, TANZANIA
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa