• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

SHINYANGA NI MKOA WA MADINI, KAMILISHENI KWA WAKATI UWANJA WA NDEGE ILI MUONGEZE FURSA - NDG. WASIRA.

Posted on: March 28th, 2025

Na. Paul Kasembo Shy RS.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (BARA) ndugu Stephen Wasira amemtaka Mkandarasi anayefanya Ukarabati Mkubwa wa Uwanja wa Ndege wa Shinyanga kukamilisha kazi hiyo kwa wakati ili uweze kuongeza fursa zaidi ukizingatia kuwa Shinyanga ni Mkoa wa Madini.

Ndugu Wasira ameyasema hayo leo Machi 28, 2025 alipotembelea uwanjani hapo ili kuona mwenendo wa ukarabati huo ambao kwa mujibu wa taarifa ya Mkandarasi China Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO) unaotarajiwa kukamilika ifikapo Juni, 2025.

"Mkoa wa Shinyanga ni Madini, naufahamu Mkoa huu ambapo ndiyo wenye madini ya Almasi kutoka hapo Mwadui, lakini tumetoka Wilaya ya Kahama ambapo kuna madini mengi ya Dhahabu na maeneo mengi hapa Shinyanga yanatoa madini, kwa hiyo kamilisheni kwa wakati ili muongeze fursa na mzunguko wa fedha kupitia uwanja huu," alisema Ndg. Wasira.

Aidha, amesema kuwa uwanja utakapokamilika yeye mwenyewe ndugu Wasira atawashawishi Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) @airtanzania_atcl ili waanze safari zao kuja Shinyanga na yeye atakuwa mmoja wa watakaokuja na ATCL katika safari yao ya kwanza hapa ili aje ashuhudie kuanza rasmi kwa matumizi ya uwanja huo unaotajwa kuwa mkombozi kwa Shinyanga na maeneo jirani.

Hii siku ya tatu ya ziara ya ndugu Wasira hapa mkoani Shinyanga ambapo alitembelea na kufanya mikutano katika Wilaya ya Shinyanga, Kahama na leo Machi 28, 2025 atamalizia na Wilaya ya Kishapu.


Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • MAISHA BAADA YA KUSTAAFU YANAHITAJI UTULIVU - DC. MTATIRO

    May 26, 2025
  • MAFUNZO YA IPOSA NI MKOMBOZI KWA VIJANA WALIO WENGI WANAOKOSA FURSA YA ELIMU YA KAWAIDA - RC. MACHA

    May 23, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa