• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

SHINYANGA RS YAFANYA KIKAO CHA MAELEKEZO YA UTEKELEZAJI NA USIMAMIZI WA MRADI WA GPE - TSP 2024/2025 KWA NGAZI YA MKOA NA HALMASHAURI ZAKE

Posted on: July 4th, 2024

Na. Paul Kasembo, SHY RS.

OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kupitia kwa Mratibu wa Mradi wa Program ya Uboreshaji Kada ya Ualimu GPE - TSP Bi. Fausta Luoga imefanya kikao na MaafisaElimu Divisheni ya Awali na Msingi , Waratibu wa mradi , Maafisa Ununuzi na Wahandisi katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri zake zote sita (6) yenye lengo la kutoa Maelekezo ya utekelezaji na usimamizi wa mradi huu unaotarajiwa kuanza rasmi Agosti, 2024.

Akizungumza wakati wa kikao hiki Bi Fausta amesema GPE TSP ni mpango unaolenga kuboresha ubora wa elimu nchini Tanzania amesema mpango huu unafadhiliwa na Ushirika wa kimataifa wa kusaidia Maendeleo ya Elimu Duniani (The Global Partnership for Education).

Malengo ya programu hii ni kuboresha ubora wa elimu, pili kuimarisha kada ya Ualimu tatu,kuongeza usawa wa kijinsi na nne, kuimarisha ujumuishi, na usimamizi wa mradi huu umegawanyika katika maeneo matatu, eneo la kwanza ni usimamizi wa programu, pili uwasilishaji wa taarifa na tatu ukusanyaji wa taarifa.

Aidha Bi. Fausta amewasisitiza waratibu kwenda kufanya vikao katika ngazi ya shule na jamii ili wawe na uelewa wa kutosha kuhusu utekelezaji na usimamizi wa mradi huku akisisitiza juu ya kuwatumia Maafisa habari na vyombo vya habari kwa lengo la kutoa habari kwa wananchi ambao kimsingi ndiyo wanufaika wa miradi hii.

"Wataalam wenzangu, twendeni tukafanye vikao na mikutano tukishirikiana na  Maafisa habari na vyombo vya habari ili kuweza kutoa habari kwa wananchi  kwa haraka, na pia kutumia mitandao ya kijamii kuielezea miradi yetu ili watu wengi wafahamu jitihada zinazofanyika na Serikali yetu ya awamu ya sita kupitia Mhe. Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan na viongozi  wengine wa Serikali yetu tukufu ili lengo la Serikali liweze kufikiwa," amesema Bi. Fausta.

Kwa upande wake muwakilishi wa Katibu Tawala Msaidizi Elimu na Ufundi ambaye pia ni Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Shinyanga Ndg. Richard Mfugale amesema kuwa shughuli zitakazotekelezwa na GPE - TSP ni pamoja na ununuzi wa vifaa visaidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum, uanzishwaji wa madarasa janja kwa ajili ya ufundishaji mubashara.

Shughuli nyingine ni uchambuzi wa hali halisi ya mifumo inayokusanya taarifa za walimu, uhusishanaji wa mifumo inayokusanya taarifa za walimu, ujenzi wa nyumba za walimu 100 na ujenzi wa vituo vya walimu 150.

Kwa Mkoa wa Shinyanga Mradi utatekeleza  ujenzi wa nyumba za walimu 18 na Vituo vya Walimu (TRC) 7, na utekelezaji wa program hii ni wa muda wa miaka minne kuanzia mwaka wa fedha 2023/2024 hadi 2026/2027.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • WANUFAIKA WA MIKOPO YA 10% LIPENI KWA WAKATI ILI PIA VIKOPESHWE NA VIKUNDI VINGINE - RC MACHA

    February 13, 2025
  • CP. HAMDUNI AKUTANA NA KAMATI YA MICHEZO YA JWTZ

    February 13, 2025
  • WANANCHI, LIPENI KODI YA ARDHI KWA WAKATI MUEPUKE RIBA - LEO KOMBA

    February 12, 2025
  • WAJUMBE WA BODI, TUMIENI TAALUMA ZENU KUISAIDIA HOSPITALI KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI- RAS CP. HAMDUNI.

    February 11, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa