Na. Paul Kasembo, KAHAMA MC.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewataka watalaam wakiongozwa na Wakurugenzi wao kubadilika na kuanza kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu zaidi wakati wote na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ili waweze kuzipunguza kama siyo kuziondoa hoja zote badala ya kusubiria wakati wa ukaguzi ili waanze kupambana kujibu wakati nafasi ilikuwepo ya kufanya hivyo awali.
RC Macha ameyasema haya leo tarehe 28 Juni, 2024 alipokuwa akifunga mkutano maalum wa baraza la madiwani katika Manispaa ya Kahama ikiwa ni hitimisho la mikutano maalum ya CAG kwa Halmashauri zote sita (6) zinazounda Mkoa wa Shinyanga huku akisisitiza umuhimu wa waheshimiwa madiwani kusimamia miradi ya maendeleo kwa wananchi wao ili waweze kuaminika na kupata hati safi za vipimo vya wananchi na wapate ridhaa tena ya kuongoza ukizingatia kuwa wananchi nao wanayo nafasi ya kupimwa kwa wananchi wao.
"Niwashauri sana wataalam wetu mkiongozwa na wakurugenzi wenu mbadilike na muanze kushirikiana kwa kufanya kazi kwa karibu zaidi wakati wote na ofisi ya CAG ili itakapofika wakati wa ukaguzi muweze kuziondoa kama siyo kuzifuta hoja zote badala ya kusubiria ufike muda wa ukaguzi ndiyo muanze kupambana kuziondoa wakati mlikuwa na hiyo nafasi kufanya kazi pamoja na kushirikiana," amesema RC Macha.
Aidha RC Macha ameitaka Manispaa ya Kahama kuhakikisha wanavipata vikundi vyote vioivyotajwa kuwa havionekani baada ya kukopa fedha kutoka kwenye mfuko wa asilimia 10 ambapo wanawake 4%, vijana 4% na watu wenye ulemavu 2% ili waweze kuzirejesha pamoja na kujibu hoja ya CAG inayotokana na madeni hayo.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mapendekezo ya CAG kwa 2022/2023 Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu ndg. Godwin Dinda kwa niaba ya Mkurugenzi ndg. Masudi Kibeto amesema kuwa Manispaa ya Kahama ilikuwa na hoja 25 ambapo hoja 9 zimejibiwa na kufungwa, huku 12 zikiwa kwenye utekelezaji, hoja 3 hazijatekelezwa na hoja 1 imejirudia.
Akiahirisha baraza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kahama Mhe. Yahaya Bundala amesema kuwa wamepokea pongezi zote kwa kupata hati safi mfululizo, wamepokea maelekezo, ushauri na mapendekezo yote yaliyotolewa na viongozi na kwamba wanakwenda kuyatekeleza kikamilifu ili mwaka wa fedha ujao wasiwe na hoja kabisa.
mh
Mstahiki Meya Manispaa ya Kahama Mhe. Yahaya Bundala
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama ndg. Masudi Kibeto
Wataalam kutoka Ofisi ya RAS - Shinyanga pamoja na Ofisi ya CAG
Sehemu ya wataalam kutoka ofisi ya Manispaa ya Kahama
Waheahimiwa madiwani Manispaa ya Kahama
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa