• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

SIKU MIA 100 ZA RAIS SAMIA

Posted on: June 27th, 2021

DKT. SENGATI ATEMBELEA MIRADI MANISPAA YA SHINYANGA KUADHIMISHA SIKU 100 ZA SERIKALI YA WAMU YA SITA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati ametembelea miradi mitatu yenye thamani ya Mil. 528 inayoendelea katika Manispaa ya Shinyanga wakati wa kuadhimisha siku 100 za uongozi  serikali ya wa wamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

 Akiongea na vyombo vya habari wakati wa ukaguzi miradi hiyo Dkt. Sengati amesema kwa kipindi cha siku 100 Rais Samia Suluhu Hasani tayari ametoa kiasi cha Shilingi Mil. 50 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Kitangiri, Mil. 50 kwa ajili ya Shule ya Sekondari Ngokoro na Mil. 428 za ujenzi daraja  linalo unganisha Kata ya Kitangili na Kata ya Chamagua zilizoko Manispaa ya Shinyanga.

Dkt. Sengati ameongeza kuwa Rais Samia alitoa fedha kwa miradi hiyo kama hatua muhimu ya kuunga juhudi za wananchi ambao tayari walishaanza juhudi za ujenzi wa miundo mbinu ya shule pamoja na Kituo cha Afya na kusema kuwa kama watu wanakuwa na uelewa kuanzisha miradi yao  serikali lazima ichangie katika juhudi izo.

‘’Kiashiria kikubwa cha Maendeleo kwa namna yoyote ile ni kiwango kikubwa cha uelewa wa wananchi, ndio maana Rais ameendelea kuwekeza katika Shule ya Msingi, Sekondari na Vyuo vya kati na vya juu kwa kuweka fedha nyingi sana hivyo tuendelee kuunga mkono jitihada hizi’’.Aliongeza Dkt. Sengati.

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa ya Iwelyangula Bw. Robert Munyereshi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuleta fedha haraka kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Iwelyangula linalounganisha Kata ya Kitangiri na Kata ya Chamagua na hivyo kuweka matumaini ya kuondokana na adha kubwa ya kukosa usafiri hasa baada ya daraja la awali kukatika na kuifanya mawasiliano yao kuwa magumu.

Mzee Munyereshi aliongeza kuwa kama Serikali itaendelea na juhudi hizi basi maendeleo ya Taifa hili yatakwenda kwa kasi sana akiwapongeza pia uongozi wa Manispaa na Wilaya kwa kuwa weledi na wenye haraka katika kushughulikia maendeleo ya wananchi.

Wakati huo Bi. Damaris Nyantabano mkazi wa Kata ya Ngokoro alimwambia Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kuwa baadhi ya wanawake jilani na Sekondari hiyo wamejitolea nguvu zao na kushiriki katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo ili kuunga juhudi za Rais Samia Suluhu hasani katika kuleta maendeleo lakini pia wanafanya hivyo kufaida ya watoto hao ambao watatumia madarasa hayo hapo baadae.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi.Yasinta Mboneko alimwambia Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kuwa miradi hiyo inayoendelea ilianza na nguvu ya Wananchi na kuweza kuinua  jengo la Kituo cha Afya na baadae Serikali kutoa kiasi cha fedha kwa ajili ya kuongezea nguvu za wananchi kukamilisha ujenzi wa miradi hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati ametembelea miradi hiyo kama hatua ya awali ya kuadhimisha siku 100 za utawala wa Rais Samia Suluhu hasani na mchango wake kwa maendeleo ya Shinyanga na Tanzania kwa ujumla.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUOMBA NAFASI YA UJUMBE WA BODI YA HOSPITALI YA MKOA January 03, 2020
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha nne 2019 January 09, 2020
  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa Kidato cha pili 2019 January 09, 2020
  • Mwenge wa Uhuru kuwasili Mkoani Shinyanga May 07, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SIKU 100

    June 27, 2021
  • SIKU MIA 100 ZA RAIS SAMIA

    June 27, 2021
  • DKT. SENGATI AHAIDI KUPAMBANA NA CHANGAMOTO YA UMASIKINI SHINYANGA

    June 05, 2021
  • Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga aapishwa

    June 02, 2021
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa