Na. Paul Kasembo, KAHAMA.
WAZIRI wa Madini Mheshimiwa Anthony Mavunde ametoa wito kwa Benki na Taasisi nyingine za kifedha nchini kuiga mfano wa CRDB Benki ya ambayo inatajwa kuwa kinara katika kufsiri maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo leo hii imetoa mfano wa Hundi yenye thamani ya Bilioni 10 kwa wachimbaji wa madini wakiwemo wadogo katika hafla iliyofanyika Manispaa ya Kahama huku akiwapongeza sana kwa utekelezaji huu wa kuigwa.
Mhe. Mavunde ameyatamka haya leo tarehe 19 Agosti, 2024 alipokuwa akikabidhi mfano wa hundi hii hafla ambayo pia imeshuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita ambaye ndiye mwenyeji wa tukio hili, viongozi mbalimbali wakiwemo na wataalam kutoka CRDB Benki wakiongozwa na mwenyeji wao ambaye pia ni Meneja Kanda ya Magharibi ndg. Jumanne Wagana (Mchumi).
"Pamoja na pongezi nyingi zaidi kwa CRDB Benki, nichukue nafasi kutoa wito kwa Benki nyingine pamoja na Taasisi zote za fedha kuiga mfano walioufanya leo CRDB Benki wa kuwapatia mkopo rahisi wachimbaji wa madini Kanda ya Ziwa Bil 10 kwa ajili ya kwenda kuimarisha shughuli zao katika maeneo wanayotoka, na hili ndiyo lengo la Serikali yetu," amesema Mhe. Mavunde.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amesema kuwa Shinyanga ni moja ya Mikoa ya kimadini ambao unatambua mchango wa Sekta ya madini na kwamba kwa mwaka 2023/2024 Mkoa ulifikisha 85% ya ukusanyaji wa maduhuli, kwa msingi huu upatikanaji wa mikopo kwa wachimbaji wadogo utachochea zaidi shughuli za uchimbaji wa madini jambo ambalo litasaidia kuongeza na kuchechemua uchumi wa wananchi na kuongeza pato la Serikali.
Mwaka 2023 Serikali kupitia kwa Mhe. Mavunde iliwaeleza watendaji wa Benki nchini juu ya changamoto ya upatikanaji wa wa huduma za kifedha ikiwemo upatikanaji wa mikopo kwa wachimbaji wadogo na kuwataka kuangalia namna ya kurahisisha upatikanaji wake ambapo leo CRDB Benki wametekeleza kwa vitendo.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa