Na Paul Kasembo, Shy Rs.
Msimamizi wa Nembo ya Jambo Group ambaye pia ni Mkurugenzi wa Jambo Fm Nickson George amesema Kampuni za Jambo zimekuwa mstari wa mbele katika kuboresha maisha ya watanzania kwani zimefanikiwa kutoa ajira kwa watu takribani 600,000 ambao wananufaika na Kampuni hizo.
Ameyasema hayo katika uzinduzi wa nembo mpya ya bidhaa za Jambo Group ambao umefanyika katika viunga vya Kampuni za Jambo Ibadakuli, Shinyanga ambapo ameeleza namna ajiri hizo zinaenda kuboresha maisha ya watanzania na kuyafanya yawe na furaha na bora zaidi.
“Sisi kama Kampuni za Jambo Group tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha tunaboresha maisha ya watanzania hususani wanashinyanga kwani mpaka sasa tumefanikiwa kuajiri watu takribani 600,000 ambao wananufaika moja kwa moja na Kampuni hizi na kupitia jaira hizi maisha yao yanazidi kuwa na furaha na bora zaidi” amesema Nickson.
Kwa nyakati tofauti viongozi wamekuwa wakitangaza na kuhamasisha wawekezaji kuja kuwekeza hapa Shinyanga.
Kwa ujumla Mkoa wa Shinyanga ni moja kati ya Mikoa yenye fursa nyingi zaidi za uwekezaji, ambapo raailimali zote zinapatikana ikiwa ni pamoja na watu, ardhi, nishati ya umeme wa kutosha, maji, miundombinu ya barabara, kiwanja cha ndege cha Kahama, kiwanja kikubwa cha ndege cha Ibadakuli inaratajiwa kukamilika, reli na usalama.
Kampuni za Jambo Group zilianzishwa mwaka 1998 na zinamilikiwa na Salum Salum ambazo zinazalisha bidhaa mbalimbali zikiwemo mikate, biskuti, maji ya kunywa pamoja, aiskrimu na zinachangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa wananchi Mkoa wa Shinyanga.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa