• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

Posted on: May 27th, 2025

#shinyanga_rs 

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga imeanza kuchukua hatua dhidi ya wote waliobainika kuhusika na ubadhirifu wa fedha zaidi ya shilingi milioni 92 zilizotengwa kwa ajili ya kuwafidia wakulima wa tumbaku kupitia Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) Ibambala kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu.

Akizungumza na waandishi wa habari Mei 27, 2025 mjini Shinyanga, Mkuu wa TAKUKURU mkoani humo, Bw. Donasian Kessy, amesema kuwa fedha hizo zilitolewa kwa ajili ya kuwasaidia wakulima waliopata hasara kufuatia mafuriko katika msimu wa kilimo wa mwaka 2023/2024. Hata hivyo, hazikuwafikia walengwa kama ilivyokusudiwa.

“TAKUKURU tumeanza kuchukua hatua kwa wote waliohusika na ubadhirifu wa shilingi zaidi ya milioni 92 zilizotengwa kwa ajili ya kuwafidia wakulima wa tumbaku wa AMCOS Ibambala,” alisema Bw. Kessy.

Kwa mujibu wa Bw. Kessy, katika kipindi cha Januari hadi Machi 2025, TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga ilipokea jumla ya taarifa 57 za tuhuma za rushwa. Kati ya hizo, taarifa 52 zilifanyiwa uchunguzi na 13 zimefikishwa mahakamani.

Katika kipindi hicho, TAKUKURU pia imefanya mikutano ya hadhara 61, semina 30, na vipindi 13 vya elimu kwa umma kupitia vituo mbalimbali vya redio na runinga, kupitia programu ya Takukuru Rafiki, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuelimisha umma kuhusu mapambano dhidi ya rushwa.

TAKUKURU inatoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na taasisi hiyo kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kupitia simu ya bure 113 au kwa kutembelea tovuti rasmi ya taasisi hiyo: www.pccb.go.tz.



Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • MAISHA BAADA YA KUSTAAFU YANAHITAJI UTULIVU - DC. MTATIRO

    May 26, 2025
  • MAFUNZO YA IPOSA NI MKOMBOZI KWA VIJANA WALIO WENGI WANAOKOSA FURSA YA ELIMU YA KAWAIDA - RC. MACHA

    May 23, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa