Na. Paul Kasembo, KISHAPU.
WAZIRI wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb) ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa amezindua Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mkoani Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine amewaeleza wananchi kuwa, kwa msimu wa kilimo cha mwaka huu wa 2024 Serikali imeleta takribani Tani Elfu 2 za mbegu ya pamba Wilaya ya Kishapu ambazo zitatolewa bure kwa wakulima wa zao la pamba zenye thamani ya zaidi ya Bilioni 2 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mfumo wa kutoa ruzuku kwa wakulima wa pamba mkoani Shinyanga.
Mhe. Bashe ameyasema haya leo tarehe 20 Novemba, 2024 wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kata ya Bubiki, Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, ambapo amehutubia mkutano huu akiwa mgeni rasmi, uzinduzi ambao umehudhuriwa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa, Wilaya, wanachama na wananchi, ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana bega kwa bega na wakulima hao wa pamba kwani mpaka sasa wameshatoa trekta 24 kati ya 30 kwa ajiri ya kuboresha, kuimarisha na kuwezesha kuwa na kilimo cha kisasa na chenye tija.
“Serikali inafanya jitihada kubwa kuboresha zao la pamba katika Wilaya ya Kishapu kwani mpaka sasa takribani Tani Elfu 2 za mbegu ya pamba zenye thamani ya Bilioni 2 zimewafikia wakulima, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mfumo wa kutoa ruzuku kwa wakulima wa pamba” amesema Mhe. Bashe.
Kwa ujumla, Wilaya ya Kishapu inatarajiwa kupokea dawa ya kuulia wadudu/ viwatilifu chupa Milioni 1 vifaa vya kilimo (trekta 30 ambapo kila kijiji kitapokea trekta 5, lakini pia kila kata kwa sasa ina Afisa Ugani Kilimo mmoja (1) wa zao la pamba huku akiahidi kwamba kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao wa 2025 mtandao wa maji ya Ziwa Viktoria utakuwa umewafikia wanabubiki na Kishapu yote kwa ujumla.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa