Na. Paul Kasembo, SHINYANGA MC.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amezishauri Halmashauri zote 6 zinazounda Mkoa kutengeneza timu maalum kwa ajili ya kushughulikia hoja mbalimbali za Mdhibiti na Mkuguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na nyinginezo kwa lengo la kuziondoa kuzipunguza kama siyo kuzifuta kabisa huku akisisitiza kuongezwa juhudi za ukusanyaji mapato na utoaji wa elimu ya wananchi kuwa na uhiari wa kulipa bila shuruti ili miradi ya Serikali iweze kutekelezeka.
RC Macha ameyasema haya leo tarehe 25 Juni, 2024 alipokuwa akitoa mchango wake katika Baraza Maalum la kujadili mapendekezo ya hoja za CAG katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambapo pamoja na kuwapongeza kwa kupata Hati Safi ya CAG lakini pia wameibuka washindi namba 1 katika mashindano ya Halmashauri Kitaifa 2024 katika Usafi wa Mji na Utunzaji wa Mazingira pamoja na kushika nafasi ya 18 Kitaifa katika utoaji wa habari dhidi ya Halmashauri 184 ushindi ambao unaiongezea morali Manispaa katika utendaji kazi wake.
"Nazishauri sana Halmashauri zote ndani ya Mkoa kuangalia namna ya kutengeneza Timu Maalum isiyozidi watu 5 pamoja na majukumu yao lakini pia kushughulikia hoja za CAG wakati wote badala ya kusubiria wakati wa ukaguzi ndiyo wataalam waanze kupambana na hoja hizi, kwa kufanya hivi Halmashauri zitapunguza kama siyo kuzimaliza kabisai," amesema RC Macha.
Kwa upande wake RAS Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo amezishauri Halmashauri kuachana na mpango wa kuanzisba miradi mipya, badala yake ishughulike na umaliziaji wa vipolo vya mwaka uliopita huku akisisitiza kuwa ni vema mradi unapoanzishwa utekelezwe mpaka mwisho kishauanzishwe mwingine, kwa kufanya hivi tija ya miradi itaonekana.
Aidha Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Nje Mkoa wa Shinyanga CPA. Yusuph Mabwe ameishauri Manispaa kuzingatia sana taratibu za kifedha na kama wanakwama popote ofisi yake ipo wakati wote kuhakikisha wanashirikiana katika kuziondoa changamoto zote.
Akiahirisha mkutano huu Mstahiki Meya Mhe. Elias Masumbuko amesema, Manispaa ilikuwa na hoja 43 ambapo 7 na 36 hazijafungwa.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa