Na. Shinyanga RS.
MKUU wa mkoa wa shinyanga Mhe. Christina Mndeme leo tarehe 19 Oktoba, 2023 amekutana na Maafisa Tarafa, watendaji wa kata, mitaa na vijiji kutoka katika Halmashauri ya Msalala, Ushetu na Manispaa ya Kahama kwa lengo la kufahamiana, kuhuisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu ya kila siku sambamba na kujadili kero na changamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi ili kuwezesha wepesi katika utumishi wao kwa wananchi wetu huku akiwataka umuhimu wa utoaji wa taatifa ya mapokezi ya fedha za miradi katika maeneo yao.
Hayo yamesemwa leo na Mhe. Mndeme katika ukumbi wa John Paul - Kahama amnapi pamoja na mambo mengine amewapongeza sana watumishi hawa kwa kazi nzuri wanazozifanya katika maeneo yao kwa ajili ya kuwaletea maendeleo jambo ambalo limekuwa likisisitizwa mara nyingi na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan huiu akiwaelekeza kwenda kusimamia vema upatikanaji wa pembejeo za kilimo kwa wakulima ili wazipate kwa wakala waliothibitishwa na mamlaka.
"Nendeni mkatoe taarifa za kukiri mapokezi ya fedha zinazoletwa kwenu kutoka serikalini kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ili wananchi wawezekujuwa kazi nzuri inayofanywa na serikali yao pamoja na utoaji taarifa wa mapato na matumizi," alisema Mhe. Mndeme.
Pamoja na mambo mengine, Mhe. Mndeme amewataka watalaam hao kwenda kuelimisha wananchi juu ya kuchukua tahadhari ya mvua za juu ya kiwango zilizotangazwa ili waondoke kwenye maeneo yote hatarishi, kuweka daftati la wageni kila mtaa na vijiji ili kudhibiti uhalifu.
Awali Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo @sizatumbo aliwataka watumishi wote kuwa na weledi, maadili, ubunifu na kufuata taratibu za kiutumishi katika kufuatilia stahiki zao.
Mhe. Mndeme amemaliza ziara ya siku mbili katika wilaya ya Kahama ambapo alikuwa na mwenyeji wake Mhe. Mboni Mhita @mboni_mhita ambapo kikao hiki kilitanguliwa na sanjo ya walinzi wa jadi wa mikoa 5 ya kanda ya ziwa iliyofanyika Kata ya Busangi - Msalala.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa