• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

TUMEKUJA KUJIRIDHISHA KAMA TARATIBU ZA MCHAKATO WA UGAWAJI WA JIMBO LA SOLWA ZILIZINGATIWA – MWITA.

Posted on: April 23rd, 2025

Na. P.aul Kasembo.

Mkurugenzi wa Daftari na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ndg. Stanslaus Mwita, amesema kuwa wamefika kujiridhisha kama taratibu na mchakato mzima wa mgawanyo wa Jimbo la Solwa ulifuatwa kulingana na maelekezo waliyotoa awali kabla ya kuanzishwa kwa zoezi hilo.

Stanslaus aliyasema hayo Aprili 23, 2025, wakati akiwasilisha taarifa ya INEC kwa wadau wa uchaguzi katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga. Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa INEC, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, na Katibu Tawala wa Mkoa huo, CP Salum Hamduni.

Wengine waliohudhuria ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mheshimiwa Peter Masindi (aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Julius Mtatiro - Wakili), Mraribu wa Uandikishaji Mkoa wa Shinyanga Ndg. Bakari Kasinyo, Waheshimiwa Madiwani, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Vyama vya Siasa pamoja na wataalamu mbalimbali wakiongozwa na Mkurugenzi wa Shinyanga DC Dkt. Kalekwa Kasanga.

"Tumekuja kujiridhisha na kuona kama taratibu na mchakato mzima wa mgawanyo wa Jimbo la Solwa ulifuatwa kulingana na maelekezo tuliyotoa kama INEC hapo awali kabla ya kuanzishwa kwa jambo hili. Hii ni sehemu tu ya mchakato, na si kwamba Tume imeridhia rasmi," alisema Mwita.

Awali, akitoa salamu za INEC, Makamu Mwenyekiti Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk alisema kuwa, pamoja na mambo mengine, uchambuzi wa kina ulifanyika kuhusu ombi hilo kwa kuzingatia vigezo muhimu ikiwemo kufanyika kwa vikao halali vya kisheria, idadi ya watu, mipaka ya kijiografia ya Jimbo la Uchaguzi, jina la Jimbo pamoja na mgawanyo wa Kata.

Nao wadau wa uchaguzi wa Shinyanga DC, akiwemo Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa Jimbo la Solwa, Ndg. Mashindike Bulanya, waliishukuru INEC kwa kuja kujiridhisha na kwamba, utekelezaji wa ugawaji wa Jimbo la Solwa unalenga kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi.


Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • MAISHA BAADA YA KUSTAAFU YANAHITAJI UTULIVU - DC. MTATIRO

    May 26, 2025
  • MAFUNZO YA IPOSA NI MKOMBOZI KWA VIJANA WALIO WENGI WANAOKOSA FURSA YA ELIMU YA KAWAIDA - RC. MACHA

    May 23, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa