Sabasaba 2025.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita @mboni_mhita mimi amewaongoza Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa kushiriki kikamilifu katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bi. Latifa M. Khamis kwenye ofisi yake iliyopo ndani ya Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) akiibeba dhamira ya dhati ya Mkoa ya kuja kuhamasisha wawekezaji zaidi kuja mkoani Shinyanga.
RC. Mboni alisema hayo Julai 4, 2025 huku akisisitiza kuwa pamoja na kuratibu ushiriki wa wafanyabiashara mkoani Shinyanga kuleta bidhaa zao katika Maonesho hayo lakini pia lengo mahsusi Ofisi yake ni kuja kuhamasisha wawekezaji kuwekeza katika Mkoa wa Shinyanga huku akitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuangazia Mkoa wa Shinyanga wwnye rasilimali nyingi na muhimu kama kitovu kipya cha fursa na maendeleo ya uwekezaji nchini.
"Sisi Mkoa wa Shinyanga pamoja na mambo mengine tumekuja katika Maonesho haya ya Sabasaba tukiwa na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa kuhamasisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja mkoani kwetu kwani tuna fursa lukuki, rasilimali zote muhimu tunazo, na kwamba tutatumia vema Maonesho haya kujitangaza Shinyanga kuwa ni Mkoa wa Kimkakati na sasa sisi Kitovu Kipya cha fursa za maendeleo ya uwekezaji nchini," alisema RC. Mboni.
Rc. Mboni Mhita @mboni_mhita anakuwa Mgeni Maalum wa siku katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba 2025 msimu wa 49 yanayofanyika katika Kiwanja cha J.K Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa