Na. Paul Kasembo, SHINYANGA DC.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kuitumia vizuri Hati Safi waliyoipata kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa ukaguzi wa mwaka 2022/2023 ili kutekeleza yale yote yaliyokuwa yamekusudiwa yakilenga pia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku akisisitiza juhudi zaidi na weledi katika kuzingatia maelekezo ya CAG ili kuendelea kupata hati safi.
RC Macha ameyasema haya leo tarehe 25 Juni, 2024 wakati wa kujadili taarifa ya hoja za CAG kwa mwaka wa fedha kuishia Juni 30, 2023 ambapo pamoja na pongezi zaidi kwa kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa jengo la Utawala ambalo kwa muda kiasi lilisimama kutokana na uzembe wa mkandarasi aliyekuwepo awali. Baada ya kumuondoa na kuweka mwingine kwa sasa ujenzi unakwenda kasi sana na umefikia hatua ya umaliziaji huku akishauri kuundwa kwa Timu ndogo ya watu (5) ambao watakuwa ni maalum kwa ajili ya kushughulikia na kujibu hoja za CAG peke yake na iwezeshwe kikamilifu kwa ajili ya kazi hii kwa lengo la kuondoa kabisa hoja zinazojitokeza
"Pamoja na kuwapongeza kwa kufanya vizuri aana na hata mkapata hati safi ya CAG, lakini nendeni mkatumie hati hiyo safi mliyoipata kutekeleza yale yote mliyoyakusudia ikiwemo kutekeleza Ilani ya CCM ambayo ndiyo inaunda Serikali yetu na ndiyo ambayo ninyi imewaajiri, hivyo zingatieni haya na mkafikie lengo mlilokusudia na siyo vinginevyo, " amesema RC Macha.
Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa CAG ndg. Thobias Shija ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Shinyanga Dkt. Kalekwa Kasanga amesema kuwa Halmashauri ilikuwa na hoja 35 za mwaka 2022/2023 na hoja za nyuma ni 69 jumla ya hoja 104 ikijumlisha na hoja za nyuma, ambapo 41 zimejibiwa na kufungwa, 47 zinaendelea na utekelezwaji, zilizofutwa ni 15 na majibu ambayo hayajakubalika ni 1.
Mwisho Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nicodemus Simoni alisema kuwa, yale yote yaliyoelekezwa wameyapokea na watayatekeleza.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa