Na. Paul Kasembo, Kahama.
MKUU wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita ameendelea na mkakati maalum wakutafsiri maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kutekeleza mambo mbalimbali ikiwemo uwezeshaji wananchi kiuchumi ambapo leo amezindua mafunzo ya Wajasiliamali wa Wilaya ya Kahama yanayohusu usindikaji, ufungaji na uokaji (Bakery & Confectionary) mafunzo ambayo yameratibiwa na Shirika la Viwango Tanzania TBS.
Pamoja na kufurahishwa kwa muitikio kwa Wajasiliamali hawa, lakini pia DC Mboni @mboni_mhita ameahidi kukutana na wafanyabiashara wa sekta zote ndani ya Wilaya ya Kahama ili kuwakumbusha na kuwaeleza fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo na Kongani katika eneo lililokuwa la Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi pamoja na kuendelea na usikilizwaji, upokeaji na utatuzi wa kero zao.
"Tutaendelea kutafsiri maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha kuwa wananchi wanafurahia maisha yao sanjari na kuwaletea maendeleo katika nyanja zote ili kuweza kutimiza malengo na matamanio yake kwa 100% ifikapo mwaka 2030," amesema DC Mboni.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa