UJUMBE wa Jumuiya ya Waislamu Ahmadiyya ukiongozwa na Sheikh Tahir Mahmood Choudhry ambaye ni Amiri na Mbashiri Mkuu wa Tanzania umefika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kujitambulisha imeingia rasmi mkoa wa Shinyanga mnamo 2018.
Pamoja na mambo mengine lakini ujumbe huu umemueleza Mkuu aa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme kuwa Jumuiya ikuwa ikifanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kujenga na kukarabati visima zaidi 100 Mkoani hapa
Aidha Jumuiya pia imejenga nyumba za Ibada pamoja na Vituo vya Walimu zaidi ya 20 ambavyo vinatumika kuelimisha wana jamii kiroho na kimwili ili kusisitiza kuishi kwa amani sawa na mafundisho ya dini tukufu ya kiislamu.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewakaribisha kwa mikono miwili huku akiwaahidi ushrikiano wa dhati kabisa wakati wote.
Kando na hayo pia Mhe. Mndeme alikumbusha juu ya umuhimu wa kuendelea kuisadia Serikali katika kukemea matendo yote yanayokuwa na mmomonyoko wa maadili kwa jamii zetu, huku akiwataka kukemea kwa nguvu zote matendo yote ya kuiga kutoka nchi za mbali ambayo yapo kinyume na tamaduni, mila na desturi zetu.
Sheikh Tahir Mahmood Choudhry ameongoza na Sheikh Abidi Mahmood Bhutt - Mkuu wa Chuo cha Jamia Ahmadiyya Morogoro na Naibu Amiri, Sheikh Abdurahman Muhammed Ame - Naibu Amiri Tanzania.
Wengine ni Ihtsham Latif - Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga, Yusuph Mgeleka - Rais wa Mkoa wa Shinyanga, Saleh Kitabu Pazi - Mwenyekiti wa Wazee wa Ahmadiyya Tanzania.@bakwatatz @ahmadiyya_tz @christinamndeme18 @johari_samizi @shinyanga_press_club
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa