Na. Paul Kasembo, SHY RS.
Umoja wa Wanawake ambao ni watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ya Shinyanga Machi 28, 2025 wametembelea na kutoa vitu mbalimbali kwa wahitaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga @shinyangarrh (Mwawaza) pamoja na Makao ya Watoto Yatima kilichopo Kata ya Lubaga, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa matendo ya huruma katika kuelekea Sikukuu ya Eid al - Fitri na Pasaka.
Akizungumza kwa niaba ya Umoja huo Afisa Utumishi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Vaileth Isack ametoa wito kwa wadau mbalimbali mkoani Shinyanga na maeneo mengine kujitokeza kushiriki matendo ya huruma kwa kuwasaidia wenye uhitaji ikiwa ni kuelekea katika Sikukuu za Eid al - Fitr na Pasaka yenye lengo la kuwapa tabasamu kwani wao ni sehemu ya jamii yetu pia.
Umoja huo umetoa mahitaji mbalimbali kama vile sabuni, mafuta, sukari, maziwa, unga wa ngano, mchele nk huku wakiwaombea kwa Mwenyezi Mungu wagonjwa wote ili wapate nafuu na wapone haraka, pia kuwatakia kila lenye kheri wale wote waliopo katika Vituo vya Malezi na wenye uhitaji kwa ujumla.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa