Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha leo tarehe 27 Mei, 2024 amekutana na viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Machinga (SHIUMA) Mkoa wa Shinyanga waliofika ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha, kufahamiana na kueleza kazi na wajibu wao kama viongozi.
Pamoja na utambulisho huu RC Macha amewakaribisha tena wakati mwingine watakapokuwa na jambo lao huku akiwasisitiza juu ya kutambua na kuthamini mchango wao katika muktadha wa kundi kubwa la wafanyabiashara ndogondogo katika Mkoa wa Shinyanga na kwamba Serikali itaendelea kushirikiana nao wakati wote.
Katika utambulisho huu wameongozana na Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Shinyanga ndg. Boniphace Petro, Makamu Mwenyekiti ndg. Mupinda Kagoma, Katibu ndg. Mwamuzi Enock na Khadija Abdallah ambaye ni mjumbe.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa