Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali imeshatafuta Mkandarasi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Ibadakuli uliopo katika Manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga atakayeanza kazi muda wowote kuanzia sasa.
Prof. Mbarawa amesema hayo alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakati wa ziara yake ya siku moja ya kukagua miradi mbalimbali inayosimamiwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Prof. Mbarawa amemtaja Mkandarasi huyo kuwa ni Kampuni ya CHICO, ambaye atakamilisha kazi hiyo baada ya mwaka mmoja na kuwa, fedha zipo tayari kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja utakaokuwa na ukubwa wa Kilometa 2.5, hivyo utakuwa ni uwanja mkubwa kwa ndege kubwa kutua.
Aidha,amesisitiza kuwa, wananchi wote wa maeneo ya Uwanja wanaostahili kulipwa fidia, watalipwa kwa mujibu wa sheria na amewataka wananchi kumpa ushirikiano mzuri Mkandarasi huyo atakapoanza kazi.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, amemueleza Prof. Mbarawa kuwa, wananchi wa Shinyanga wana shauku kubwa kuona uwanja wa ndege wa Ibadakuli unakarabatiwa na unafanya kazi.
Mhe. Telack pia amemuomba Waziri Mbarawa kusaidia usimamizi wa Ujenzi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa inayojengwa katika eneo la Mwawaza Manispaa ya Shinyanga, pamoja na Hospitali ya Wilaya ya Kahama inayotarajiwa kujengwa.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa