• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

Viongozi na Watendaji wapata dozi ya kujiepusha na mgongano wa maslahi

Posted on: January 11th, 2020

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovela amewataka viongozi na watendaji kuzingatia suala la uadilifu katika utendaji wa shughuli za Umma ili kuepukana na madhara yanayotokana na mgongano wa maslahi.

Akifungua mafunzo ya sheria ya maadili ya utendaji katika utumishi wa Umma na namna bora ya kujiepusha na mgongano wa maslahi kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Shinyanga, yaliyofanyika jana tarehe 10/01/2020 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Msovela amesema kuwa, ana imani kubwa baada ya mafunzo hayo yenye lengo la kukumbushana kuzingatia Sheria, taratibu na kanuni, washiriki watasimamia vema kwenye maeneo yao ya kazi.

"Hivyo mafunzo haya yanasisitiza katika kutekeleza majukumu yetu kusimamia sheria za Nchi, haki na utu ili kumsaidia mhe. Rais katika kutekeleza majukumu yake na hatimaye kutoa huduma bora kwa jamii" amesema Msovela.

Amesema kuwa tofauti na miaka ya nyuma, suala la mgongano wa maslahi limepungua kwa kiasi kikubwa.

Aimeipongeza pia Sekretarieti ya maadili kwa Viongozi wa Umma chini ya Kamishna Jaji mstaafu Nsekela kwa kuendesha mafunzo haya ili kujenga uelewa kwa viongozi hasa katika Mkoa wa Shinyanga tangu mwezi Juni, 2019 kwa njia mbalimbali.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Gulamhafidh Mukadam aliyeshiriki pia mafunzo hayo amesema mafunzo yanawakumbusha na kuwakosoa pale walipokwenda kinyume na kumshukuru Rais  Magufuli kwa utendaji wake ambapo amesema kuwa ni kweli nchi imebadilika sana. 

Mmoja wa washiriki Bw. Nila Mabula ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa ndani katika Sekretarieti ya Mkoa, akitoa neno la shukrani baada ya mafunzo, amesema kuwa wanaishukuru sana Sekretarieti kwa mafunzo hayo na kuwasihi washiriki kuyazingatia na kuyashusha kwa watumishi wa chini ili kufikia lengo. Akiongeza kuwa, faida yake ni kuongeza ufanisi katika kazi kwenye nyanja zote.

"Kanuni tulizotajiwa zimetajwa pia hata kwenye vitabu vya dini, hivyo kuzingatia ni kufuata pia maneno ya Mungu" amesema Bw. Nila.

Viongozi na watendaji mbalimbali ngazi ya Mkoa wameshiriki mafunzo hayo ya siku moja wakiwemo Wakuu wa vyombo vya Usalama, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Makatibu Tawala wa Wilaya, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Idara na Vitengo, watendaji wa Mahakama na Wakuu wa Taasisi za Umma.





Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • MAISHA BAADA YA KUSTAAFU YANAHITAJI UTULIVU - DC. MTATIRO

    May 26, 2025
  • MAFUNZO YA IPOSA NI MKOMBOZI KWA VIJANA WALIO WENGI WANAOKOSA FURSA YA ELIMU YA KAWAIDA - RC. MACHA

    May 23, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa