Na, Shinyanga MC
WAANDIKISHAJI wa Orodha ya Wapiga Kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wameapishwa kiapo cha Kutunza Siri pamoja na Kiapo cha Utii na Uadilifu
Uapisho huu umefanyika leo Oktoba 8,2024 katika ukumbi wa mikitano Chuo cha Ualimu Shinyanga SHYCOM.
Akizungumza mara baada ya kuapishwa kwa Waandikishaji hao,Msimamizi Msaidizi Ngazi ya jimbo Bw.Charles Kafutila amewataka wasimamizi hao kuwa na Lugha nzuri kwa wananchi ili wananchi waweze kujiandikisha kupiga kura wakati wa uchaguzui ikiwa ni haki yao ya msingi.
“leo mmeapishwa hapa kiapo cha kutunza siri Pamoja na kiapo cha uaminifu, ni Imani yangu kuwa kama serikali ilivyowaamini na kuwateuwa kusimamia zoezi hili ndivyo hivvyo muende kutimize majukumu yenu, nendeni mkaongee lugha rafiki kwa wananchi ili waweze kujitokezaa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa. Amesema Bw. Kafutila
Zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 linatarajiwa kuanza kufanyika 11-10 Oktoba 2024. Huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika Novemba 27,2027 ambapo kwa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Jumla ya wakazi 120,345 wanatarajiwa kuandikishwa kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa