Na. Shinyanga RS.
Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga imefika kwa Mkuu wa Mkoa kutambulisha rasmi Kamati ya Kushughurikia Malalamiko na Kero kuhusu Maji ngazi ya Mkoa ambayo itakuwa na jumla ya wajumbe 10.
Akizungumza wakati wa kikao cha utambulisho huo Meneja RUWASA Mkoa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovera alisema kwamba kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali ni kwamba kunakuwa na Kamati kuanzia ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya na Mkoa ambapo leo ndiyo rasmi Kamati inatambukishwa hapa ambapo Mwenyekiti wake ni Mkuu wa Mkoa.
"Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, tumefika hapa kwa lengo la kuitambulisha rasmi kwako Kamati ya Mkoa ambayo kwa mujibu wa sheria Mkuu wa Mkoa (Mhe. Christina Solomon Mndeme) ndiye Mwenyekiti wa Kamati," alisema Eng. Julieth.
Akiwasilisha maelezo ya lengo la mwongozo huo kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ambaye ni Afisa Maendeleo RUWASA Ndg. Rashid Ngoya alisema kuwa Lengo Kuu la Mwongozo wa Kutatua Malalamioo ni kupokea, kutathimini na kutatua malalamiko hayo yanayohusiana na mradi kutoka katika ngazi zote za jamii zilizoathirika na kutoa fursa kwa wadau wa mradi kuwasilisha maswali, maoni, kero, mapendekezo na malalamiko.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hii ya Malalamiko Mhe. Christina Mndeme pamoja na kuwashukuru RUWASA kwa utambulisho wa Kamati lakini akatoa maelekezo kwa wajunbe walioteuliwa kuwa wanahudhuria vikao wao wenyewe siyo kutuma wawakilishi.
Maelekezo mengine ni kuwa, Sekretarieti kuwasilisha kabrasha mapema kabla ya kikao ili waweze kusoma na kuelewa, kuwepo na Rejesta Maalumu ya malalamiko inayoonesha ni idadi ngapi ya malalamiko yamepokelewa / yaliyoshughurikiwa na mwisho akawataka wajumbe kutatua malalamiko kwa uwazi zaidi.
Kwa ujumla, uwepo wa kamati hii panoja na majukumu mengine kutakwenda kutoa elimu kubwa zaidi kwa jamii itambue kuwa katika utekelezaji wa miradi hii hakutakuwa na fidia ya aina yoyote kwa mtu ambaye mradi unatekelezwa kwenye eneo lake.
@ortamisemi @christinamndeme18 @ruwasa_shinyanga @shinyanga_press_club
|
ReplyForward
|
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa