• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

WAKULIMA, LIONGEZEENI THAMANI ZAO LA CHOROKO – RC MACHA

Posted on: April 3rd, 2025

Na. Paul Kasembo, Shinyanga DC.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewataka Wakulima wa Kijiji cha Mwamakaranga, Kata ya Iselamagazi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kukipa kipaumbele kilimo cha zao la choroko na kulifanya kuwa zao la kibiashara ili kuongeza thamani yake na kuwawezesha kunufaika zaidi na zao hili ambalo linazidi kukua kwa kasi.

RC Macha ameyasema haya leo Aprili 3, 2025 wakati wa mkutano wa hadhara na wakulima wa Mwamakaranga ambapo ulilenga kuonana, kujadili na kupata ufumbuzi wa changamoto wanazopitia wakulima hao sanjari na RC Macha kutembelea Ghala la kuhifadhi nafaka la Katemi lililopo kijijini hapo na  kuona ufanisi wa kazi zake.

“Niwaombeni ndugu zangu Wakulima, pamoja na kulima mazao mengine lakini nawasisitiza sana mkipe kipaumbele kilimo cha zao la choroko na kulifanya zao hili kuwa la kibiashara zaidi ili kuliongezea thamani yake kwa kufanya hivyo kutawawezesha ninyi kunufaika zaidi kwani zao hili linazidi kukua kwa kasi sana hivi sasa” amesema RC Macha.

RC Macha pia ametumia nafasi hiyo kuwasisitiza kujisajili na kutumia Mfumo wa Stakabadhi Ghalani ambao unalenga kumnufaisha zaidi mkulima kwani mpaka sasa umeonesha waziwazi bei halisi ya zao husika na hivyo kumuepusha mkulima na walanguzi ambao wamekuwa wakiwakandamiza kutokana na bei zisizo halali.

Aidha ameongeza kuwa Serikali inakuja na utaratibu wa kuhakikisha zao la choroko linauzwa na kununuliwa kwenye maghala yaliyosajiliwa na yanayosimamiwa vizuri kwani hamu ya Serikali ni kuona wakulima ndio wanakuwa wanufaika wakubwa zaidi wa zao hili na mazao mengine ya kibiashara kuliko wafanyabiashara ambao kwa sasa ndio wanaonufaika zaidi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Julius Mtatiro (Wakili) amepokea maagizo ya RC Macha na kuahidi kuwa atashirikiana bega kwa bega na wakulima hao kuhakikisha zao la choroko linasonga mbele na kuleta maendeleo chanya kwa wakulima

Akihitimisha ziara yake RC Macha amewaomba na kuwasisitiza wakulima kuendelea kushirikiana kwa pamoja na Vyama vya Ushirika vya Kilimo na Masoko (AMCOS) ili kuliinua zao hili na kulifanya lizidi kupaa kimataifa.


Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • MAISHA BAADA YA KUSTAAFU YANAHITAJI UTULIVU - DC. MTATIRO

    May 26, 2025
  • MAFUNZO YA IPOSA NI MKOMBOZI KWA VIJANA WALIO WENGI WANAOKOSA FURSA YA ELIMU YA KAWAIDA - RC. MACHA

    May 23, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa