• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

Wakuu wa shule watakiwa kusimamia Taaluma badala ya kushinda kwenye Ofisi za Halmashauri

Posted on: February 4th, 2020

Wakuu wa shule za Msingi na Sekondari Mkoani Shinyanga wametakiwa kusimamia ufundishaji na ujifunzaji katika shule zao badala ya muda mwingi kuutumia kwenye Ofisi za Halmashauri.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack mapema leo tarehe 04 Februari, 2020 kwenye kikao cha pamoja na Wakuu wa shule za Msingi na Sekondari, Maafisa Elimu kata na Watendaji wa kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, kilichofanyika katika shule ya sekondari Mwalimu Nyerere ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa shughuli za elimu Wilaya ya Kahama,.

Mhe. Telack ambaye amefanya ziara katika baadhi ya shule hapo jana tarehe 03/02/2020 kabla la kikao hicho amebaini changamoto mbalimbali ikiwemo Wakuu wa shule kutofuatilia hali ya ufundishaji shuleni kuanzia kwa walimu hadi wanafunzi hali iliyochangia kushuka kwa ufaulu.

“Rudini mkasimamie ufundishaji na ujifunzaji, nataka tutoke hapa tulipo. Wakuu wa shule badilikeni, fungueni milango ofisi zenu ziwe rafiki kwa walimu, wazazi na wanafunzi. Maafisa Elimu hakuna kuita Wakuu wa shule Halmashauri waacheni wasimamie taaluma kwenye shule zao ” amesisitiza Telack.

Aidha, amewataka Wakuu wa shule kujiepusha na urafiki katika kazi ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima badala yake wahakikishe kunakuwa na mahusiano mazuri ya kikazi.

Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya elimu, ambaye ni Afisa elimu Mkoa Bw. Mohamed Kahundi amewataka Wakuu wa shule kuhakikisha wanakuwa na miongozo yote inayohitajika ili kuwasaidia kufuatilia ufundishaji.

Nao baadhi ya Walimu wakuu na Maafisa elimu kata wamemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuyafanyia kazi yale yote aliyowaelekeza na  kumuomba kuwasaidia kupunguza changamoto zinazowakabili ikiwemo uhaba wa walimu, miundombinu na kutopandishwa madaraja kwa wakati.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza na Walimu Wakuu, Maafisa elimu wa kata na Watendaji wa kata (Hawapo pichani) wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala leo tarehe 04/ 02/2020 katika ukumbi wa shule ya sekondari Mwalimu Nyerere

Baadhi ya washiriki wa kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Watendaji wa kata, Maafisa Elimu kata na Walimu Wakuu wa shule za msingi na sekondari wakimsikiliza kwa makini (hayupo pichani) leo katika ukumbi wa shule ya sekondari Mwalimu Nyerere

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha (kushto), katika shule ya sekondari Isaka, Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Wilaya ya Kahama wakikagua nyaraka za maandalio ya masomo kwenye ofisi ya walimu

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akimuhoji mtoto James Jeremia aliyedai hawezi kusoma licha kufaulu mtihani wa darasa la saba na kupelekwa shuleni na baba yake Bw. Jeremia James hapo jana tarehe 03/02/2020 katika shule ya sekondari Mwakata. Mhe. Telack ameagiza mtoto huyo aanze masomo shuleni hapo mara moja

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamringi Macha akitoa neno kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kulia) kuzungumza na walimu Wakuu, Maafisa Elimu kata na Watendaji wa kata Halmashauri ya Wilaya ya Msalala

Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Elimu Bw. Mohamed Kahundi, akizungumza katika kikao hicho leo tarehe 04/02/2020

Mwalimu Dotto Mayiga wa shule ya msingi Kakola B, akizungumza katika kikao hicho

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • WANUFAIKA WA MIKOPO YA 10% LIPENI KWA WAKATI ILI PIA VIKOPESHWE NA VIKUNDI VINGINE - RC MACHA

    February 13, 2025
  • CP. HAMDUNI AKUTANA NA KAMATI YA MICHEZO YA JWTZ

    February 13, 2025
  • WANANCHI, LIPENI KODI YA ARDHI KWA WAKATI MUEPUKE RIBA - LEO KOMBA

    February 12, 2025
  • WAJUMBE WA BODI, TUMIENI TAALUMA ZENU KUISAIDIA HOSPITALI KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI- RAS CP. HAMDUNI.

    February 11, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa