• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI NDANI YA MKOA WA SHINYANGA, HAKIKISHENI MASOKO YOTE YANAKUWA SAFI WAKATI WOTE - RC MACHA.

Posted on: September 20th, 2024

Na. Paul Kasembo, SHY RS.

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote ndani ya Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha kuwa masoko na magulio yote yanafanyiwa usafi na kuwa safi wakati wote kwa kuwa kwa sehemu kubwa ndiyo kunapatikana vyakula ambavyo tunakula lakini pia kwa sehemu kubwa ndiyo kwenye mkusanyiko wa watu wengi zaidi.

RC Macha ameyasema haya leo tarehe 20 Septemba, 2024 wakati alipoongoza wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kusafisha mazingira katika soko la Nguzonane lililopo Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Usafishaji Duniani ambapo kwa Mkoa wa Shinyanga yamefanyika hapa Manispaa ya Shinyanga. 

"Nitumie nafasi hii kuwaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote ndani ya Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha kuwa masoko na magulio yote katika maeneo yao yanafanyiwa usafi na kuwa safi wakati wote kwakuwa kwa sehemu kubwa ndiyo maeneo ambayo chakula kinapatikana na ndiyo kwenye mkusanyiko wa watu wengi zaidi," amesema RC Macha.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni ambaye ameongoza watumishi wengine wote, Taasisi, Vyombo vya Usalama na wadau wa usafi mkoani Shinyanya amesema kuwa Siku ya usafishaji Duniani (WORLD CLENAUP DAY) chimbuko lake ni huko ESTONIA iliyopo Ulaya Kaskazini ambapo asilimia 4 ya watu walijitokeza pasipo shuruti ya serikali kufanya usafi wa mazingira nchi nzima kwa masaa kadhaa tu, jambo hili lileta muamko na mvuto wa kipekee kwa jamii nzima na serikali, likapata kibali sana, wakati huo liliongozwa na kauli mbiu “NCHI MOJA, SIKU MOJA”. 

"Jambo hili halikubaki kuwa siri tena kwa watu wa Estonia tu bali lilileta muamko wa kihisia na kupokelewa na jamii mbalimbali Duniani kwa kuja na msemo wa “DUNIA, TUFANYE” (Let’s Do it! World), na hapo jambo likaunganisha watu kutoka pande zote za Dunia na kuamua kuwa na siku maalumu ya usafi ambayo ni tarehe 20 septemba. Siku hii haijabaki kama siku ya kuondoa taka ngumu tu bali ni siku ya kimkakati wa kutokomeza magonjwa ya mlipuko yanayotokana na uchafu na kwa Tanzania maadhimisho haya yameanza kuadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2018 na kuanzia hapo kila ifikapo tarehe 20 Septemba kama leo huwa ni maadhimisho yake," amesema RAS CP. Hamduni.

Usafi ni suala nyeti linalomgusa kila mtu. Usafi unayagusa maisha yetu ya kila siku, mbali na kwamba ni ustaarabu lakini linachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza magonjwa ya kuambukiza na mlipuko yanayotokana na uchafu wa mazingira kama vile Magonjwa ya mfumo wa upumuaji, Kuhara damu, Minyoo, Malaria n.k.

Kauli mbiu ya maadhimisho haya inasema "Uhai Hauna Mbadala, Zingatia Usafi wa Mazingira".

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • WANUFAIKA WA MIKOPO YA 10% LIPENI KWA WAKATI ILI PIA VIKOPESHWE NA VIKUNDI VINGINE - RC MACHA

    February 13, 2025
  • CP. HAMDUNI AKUTANA NA KAMATI YA MICHEZO YA JWTZ

    February 13, 2025
  • WANANCHI, LIPENI KODI YA ARDHI KWA WAKATI MUEPUKE RIBA - LEO KOMBA

    February 12, 2025
  • WAJUMBE WA BODI, TUMIENI TAALUMA ZENU KUISAIDIA HOSPITALI KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI- RAS CP. HAMDUNI.

    February 11, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa