Na. Paul Kasembo, SHY RS.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewaasa walengwa wanaonufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) Mkoa wa Shinyanga ambao wamefikia hatua ya kuhitimu na mpango huu kuwa tayari kuwaachia wanufaika wengine ili na wao pia wanufaike.
RC Macha ameyasema haya leo tarehe 7 Novemba, 2024 wakati akifungua Kikao Kkazi cha kujenga uelewa kuhusu utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini kwa viongozi na waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Kagera na Geita kikao ambacho kimefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
“Ndugu zangu wanahabari, malengo makubwa ya TASAF ni kuhakikisha wanawasaidia walengwa ambao watajinusuru na umaskini na msingi huu sasa, walengwa wote ambao kwa sasa wananufaika na tayari wamehitimu tayari wawe tayari kuwaachia na wengine ili nao wanufaike na mpango huu na hatimae waweze kuondokana na umaskini na mwisho wajikwamue kiuchumi wao na familia zao na ndiyo lengo hasa la Serikali,” amesema RC Macha.
Aidha RC Macha ameongeza kuwa lengo kubwa la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na uongozi wake ni kuhakikisha kuwa Watanzania wote wanaishi katika hali nzuri ya kiuchumi na kwa ustawi sawa na hatimaye kuondokana na umaskini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mfumo wa Mawasiliano TASAF Makao Makuu Ndg. Japhet Boaz amesema kuwa kufikia Juni 2024 jumla ya vikundi 60,342 Tanzania nzima vyenye wananchama 838,241 vimefanikiwa kukusanya akiba ya shilingi Bilioni 7.9 na kukopeshana shilingi Bilioni 3.2 kwa ajiri ya kuanzisha na kuendeleza miradi mbalimbali inayowaongezea kipato ili kukuza uchumi wa kaya.
Aidha ameongeza kuwa kaya za walengwa 84,674 zimepewa mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa biashara na kupatiwa ruzuku ya uzalishaji ambapo mpaka sasa wameanzisha shughuli za kiuchumi zenye thamani ya shilingi Bilioni 31.3 na hivyo kufanikiwa kuhitimu kwenye mpango wa kaya maskini ili kuwapisha wengine wanufaike na mpango huu.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa