Jumla ya wanafunzi 1352 waliosajiliwa kufanya mtihani wa Taifa wa kidato cha sita katika Mkoa wa Shinyanga, wameungana na wenzao nchini kufanya mtihani huo ulioanza leo tarehe 07 Mei, 2018.
Taarifa kutoka Sehemu ya huduma za Elimu katika Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga, kuna shule 13 za Sekondari katika Mkoa wa Shinyanga zenye kidato cha Sita. Aidha, kati ya wanafunzi hao 1352, wanafunzi 1247 ni wale wa shule za Serikali na wanafunzi 105 wa shule za Binafsi.
Mtihani huo unafanyika sambamba na mtihani wa Ualimu ambapo kwa Mkoa wa Shinyanga kuna chuo kimoja cha Ualimu cha "Shinyanga Teacher's College" kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga chenye wahitimu 26 watakaofanya mtihani.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa