Repost @SHINYANGA PRESS CLUB BLOG
WANAHABARI Mkoa wa Shinyanga kupitia Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) wametembelea Bustani ya Wanyama maarufu Jambo Zoo iliyopo Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga, inayomilikiwa na Kampuni ya Jambo Group.
Ziara hiyo imefanyika leo Aprili 19, 2025 ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhamasisha utalii wa ndani pamoja na kuwaunga mkono wawekezaji wazawa, ambapo imeratibiwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mhifadhi wa Jambo Zoo ndg. Babuu Burhan Kajuna alisema bustani hiyo ina wanyama wa aina mbalimbali ambao wamepewa mafunzo na kuzoea binadamu, hivyo kuwawezesha wageni kupiga nao picha kwa ukaribu.
"Tunawashukuru waandishi wa habari kwa kutembelea Jambo Zoo. Tunawakaribisha wananchi wote waje kufanya utalii wa ndani hapa Shinyanga. Bei zetu ni rafiki kabisa – watu wazima ni shilingi 20,000 na watoto shilingi 10,000," amesema Kajuna.
Ameongeza kuwa wageni wanaofika katika bustani hiyo hupata fursa ya kujifunza kuhusu tabia za wanyama, kupiga nao picha kwa ukaribu, na kuwalisha chakula kwa mikono yao.
Kwa upande wake, Msimamizi wa Chapa kutoka Jambo Group Nickson George, amewataka wananchi kuitembelea bustani hiyo hasa katika kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka, wakiwa na familia zao, huku wakifurahia vinywaji vipya vya Jambo Lemon Lime na Jambo Power Boom.
Aidha, Mratibu wa ziara hiyo, Marco Maduhu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Tendaji ya SPC na mfadhili wa safari hiyo, ameipongeza Kampuni ya Jambo Group kwa uwekezaji wa bustani hiyo ya wanyama, akisema umeunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha utalii wa kupitia filamu ya The Royal Tour.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa