• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

WANAHABARI, TUMIENI MAFUNZO YA M-MAMA KUWASAIDIA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA –MLYUTU

Posted on: November 5th, 2024

Na. Paul Kasembo, SHY RS.

MWAKILISHI  wa Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Daktari. Faustine Mulyutu amewaasa wanahabari ambao wamehudhuria mafunzo haya ya m-mama kutumia vizuri yale waliyojifunza kuijulisha jamii juu ya utoaji na utumiaji wa namba 115 ili kuhakikisha inaenda kutengeneza afya ya mama na mtoto pindi dharula inapotokea.

Ameyasema haya tarehe 5 Novemba, 2024 wakati akizungumza na wanahabari kutoka Redio za Kijamii mbalimbali zilizopo ndani ya Mkoa wa Shinyanga, Tabora, Simiyu na Kigoma kwenye mafunzo ya huduma ya usafirishaji wa dharula kwa wajawazito waliojifungua ndani ya siku 42 na watoto wachanga ndani ya siku 28 (m-mama) ambayo yamefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Vigimark iliyopo Manispaa ya Shinyanga.

“Wanahabari na vyombo vyenu vya kutolea habari mnayo nafasi kubwa sana ya kuisaidia jamii kuelewa vizuri na kwa undani kuhusu huduma ya m-mama ambayo inalenga kuwasaidia akina mama wajawazito na watoto wao wachanga pindi wanapopata dharula na kuhitaji matibabu, hivyo mtumie mafunzo haya kwenda kuwasaidia kufikisha elimu ya matumizi sahihi ya kupiga 115 ambayo ni bure ili wapate msaada wanapouhitaji” amesema Mlyutu.

Aidha amemuomba mratibu wa mafunzo ya m-mama Mkoa wa Shinyanga kuandaa ratiba ya waratibu wa huduma ya afya ili watimize jukumu la utoaji wa elimu ya afya kupitia redio za jamii ili kufikisha ujumbe kwa wanajamii kuhusu huduma hii ya dharula  kwa mikoa yote 4 iliyoshiriki mafunzo huku Shinyanga ikitajwa kuwa ya kwanza kutembelewa.

Akiwasilisha mafunzo kwa wanahabari, Mratibu wa mfumo wa m-mama ambaye pia ni Muuguzi Mkuu Mkoa wa Shinyanga Bi. Flora Kajumulla amesema mfumo wa m-mama umetengenezwa kuwa endelevu na nafuu zaidi kwani Serikali imeanzishwa dawati la msaada mtandaoni kwa kila Mkoa nchini ili kuripoti matatizo yoyote ya m-mama huku madereva 4000 tayari wamesajiriwa kutoa huduma ya usafiri.

Huduma ya m-mama inapatikana bure sehemu popote Tanzania kwa kupiga namba 115 ili kuwasiliana na waratibu wa mfumo wa m-mama ambapo mpaka sasa zaidi ya rufaa za akina mama 80,000 na watoto wachanga 17,750 zimesafirishwa.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAPITIO YA ROBO MWAKA KWA KIPINDI CHA OKT - DES 2024 CHA (PJT MMMAM) CHAFANYIKA MKOANI SHINYANGA.

    February 28, 2025
  • RCC SHINYANGA YARIDHIA MAPENDEKEZO NANE (8) YA MATUMIZI BORA YA ARDHI.

    February 27, 2025
  • KUKAMILISHWA KWA MIRADI YA BARABARA KUTAPUNGUZA KERO KWA WANANCHI – RC MACHA

    February 26, 2025
  • WALIMU, TOENI ELIMU INAYOENDANA NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA -RC MACHA

    February 24, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa