Na. Paul Kasembo, Kishapu.
WANANCHI Wilayani Kishapu wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuimarisha kazi ya kulinda raia na mali zao jambo ambalo limepelekea kuongeza mzunguuko wa fedha kwakuwa hivi sasa wanafanya kazi bila hofu na kiongeza masaa zaidi ya kutekeleza majukumu yao ambayo yanaboresha maisha yao kiuchumi.
Pongezi hizi zimetolewa tarehe 23 Mei, 2024 na wananchi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha wakati akifungua soko rasmi soko la Pamba katika Wilaya ya Kishapu baada ya kuanza kusikiliza na kutatua kero za wananchi, ambapo wananchi wamekiri na kupongeza kwa dhati kuwa Jeshi la Polisi limekuwa na msaada mkubwa kwao.
RC Macha Mhe. Macha kwa nyakati tofauti amekuwa akilipongeza sana Jeshi la Polisi na hususani RPC Shinyanga SACP Janeth Magomi, na wasaidizi wake wote kwa namna ambavyo anaridhishwa na utekelezaji wa majukumu yao. RC Macha amesisitiza kuwa kasoro zilizopo katika Jeshi la Polisi ni za mtu mmoja mmoja na siyo Jeshi lote na kwamba Jeshi la Polisi ni safi na utendaji kazi wake unaridhisha na hauna shaka kabisa kama ambavyo wananchi wa Kishapu walivyokiri, kuthibitisha na kupongeza wao wenyewe baada ya kuridhishwa ambapo pongezi hizi zimepokelewa na ASP Samwel Joseph, ambaye ni Operasheni Ofisa Wilaya ya Kishapu kwa niaba ya OCD.
"Kwa dhati kahisa na kwa niaba ya wananchi wenzangu tunalipongeza sana Jeshi la Polisi hapa Wilayani Kishapu, kwa kweli wanafanya kazi nzuri sana matukio hamna tena na amani sasa ipo ya kutosha muda wote kwa hili tunawapongeza sana," amesema Charles Mashenene mkazi wa Kishapu.
RC Macha anaendelea na ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri zote sita (6) na Wilaya zote tatu (3) ambapo leo anafungua msimu wa soko la pamba katika Vyama vya Ushirika vilivyopo Wilaya ya Kishapu na baadae atakagua upanuzi wa mnada wa Mhunze kisha atafanya mkutano wa hadhara kupokea, kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika mnada wa Mhunze.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa